1 Mambo ya Nyakati 28

Maandalizi Ya Daudi Ya Kujenga Hekalu

1 Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na maaskari wote walio hodari.

2 Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano laBwanakwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga.

3 Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’ ”

4 “Hata hivyoBwana, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka katika nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka katika wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote.

5 Miongoni mwa wanangu wote, nayeBwanaamenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme waBwanajuu ya Israeli.

6 Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake.

7 Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’

8 “Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili laBwananaye Mungu wetu akiwa anasikia: Iweni na bidii kuzifuata amri zaBwanaMungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.

9 “Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maanaBwanahuuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako, bali kama ukimwacha, yeye atakukataa wewe milele.

10 Angalia basi, kwa maanaBwanaamekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.”

11 Ndipo Daudi akampa mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.

12 Akampa vielelezo vya yote ambavyo Roho alikuwa ameweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu laBwanana vyumba vyote vinavyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

13 Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu laBwana. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu.

14 Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali.

15 Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara,

16 uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha,

17 uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia, uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu, uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha

18 na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano laBwana.

19 Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwaBwanaulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.”

20 Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maanaBwanaaliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu laBwanaitakapokamilika.

21 Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yo yote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/28-fb2a62e57b75a2d056b8241069adae59.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × four =