1 Samweli 12

Hotuba Ya Samweli Ya Kuaga

1 Samweli akawaambia Israeli wote, “Nimesikiliza kila kitu mlichoniambia nami nimewawekea mfalme juu yenu.

2 Sasa mnaye mfalme kama kiongozi wenu. Lakini kwa habari yangu mimi ni mzee na nina mvi, nao wanangu wapo hapa pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu mpaka siku hii ya leo.

3 Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni juu yangu mbele zaBwanana mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Ni nani nimepata kumwonea? Ni kutoka kwenye mkono wa nani nimepokea rushwa ili kunifanya nifumbe macho yangu? Kama nimefanya cho chote katika hivi, mimi nitawarudishia.”

4 Wakajibu, “Hujatudanganya wala kutuonea. Hujapokea cho chote kutoka kwenye mkono wa mtu awaye yote.”

5 Samweli akawaambia, “Bwanani shahidi juu yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta cho chote mkononi mwangu.”

Wakasema, “Yeye ni shahidi.”

6 Kisha Samweli akawaambia watu, “Bwanandiye aliyemchagua Mose na Aroni na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri.

7 Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu ninakwenda kukabiliana nanyi kwa ushahidi mbele zaBwanakwa matendo yote ya haki yaliyofanywa naBwanakwenu na kwa baba zenu.

8 “Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimliliaBwanakwa ajili ya msaada, nayeBwanaakawatuma Mose na Aroni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa.

9 “Lakini wakamsahauBwanaMungu wao, hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori na katika mikono ya Wafilisti na mfalme wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao.

10 WakamliliaBwanana kusema, ‘Tumetenda dhambi; tumemwachaBwanana kutumikia Mabaali na Maashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka katika mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia.’

11 NdipoBwanaakawatuma Yerub-Baali, Baraka, Yeftha na Samweli, naye akawaokoa kutoka katika mikono ya adui zenu kila upande, ili ninyi mpate kukaa salama.

12 “Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawaBwanaMungu wenu alikuwa mfalme wenu.

13 Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni,Bwanaamemweka mfalme juu yenu.

14 Kama mkimchaBwanana kumtumikia na kumtii nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayetawala juu yenu mkimfuataBwana, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu!

15 Lakini kama hamkumtiiBwana, nanyi kama mkiasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu.

16 “Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambaloBwanaanakwenda kulifanya mbele ya macho yenu!

17 Je, sasa si mavuno ya ngano? NitamwombaBwanaili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho yaBwanamlipoomba mfalme.”

18 Kisha Samweli akamwombaBwana, na siku ile ileBwanaakatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sanaBwanana Samweli.

19 Watu wote wakamwambia Samweli, “MwombeBwanaMungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”

20 Samweli akajibu, “Msiogope, mmefanya uovu huu wote; hata hivyo msimwacheBwana, bali mtumikieniBwanakwa moyo wenu wote.

21 Msigeukie sanamu zisizofaa. Haziwezi kuwatendea jema, wala haziwezi kuwaokoa kwa sababu hazina maana.

22 Kwa ajili ya jina lake kuuBwanahatawakataa watu wake, kwa sababu ilimpendezaBwanakuwafanya kuwa wake mwenyewe.

23 Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi yaBwanakwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka.

24 Lakini hakikisheni mnamchaBwanana kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote, tafakarini ni mambo gani makubwa aliyotenda kwa ajili yenu.

25 Hata hivyo mkiendelea kufanya uovu, ninyi na mfalme wenu mtafutiliwa mbali!”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1SA/12-3d7adcdded84140c77aa14094ce7e3b8.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nine − five =