1 Samweli 3

Bwana Amwita Samweli

1 Kijana Samweli alihudumu mbele zaBwanachini ya Eli. Katika siku zile neno la Mungu lilikuwa adimu, hapakuwepo na maono mengi.

2 Usiku mmoja Eli, ambaye macho yake yalikuwa yamefifia sana kiasi kwamba aliona kwa shida sana, alikuwa amelala mahali pake pa kawaida.

3 Taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala HekalunimwaBwana, ambapo Sanduku la Mungu lilikuwako.

4 KishaBwanaakamwita Samweli.

Samweli akajibu, “Mimi hapa.”

5 Naye akakimbia kwa Eli na kumwambia, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Lakini Eli akasema, “Sikukuita; rudi ukalale.” Hivyo akaenda kulala.

6 Bwanaakaita tena, “Samweli!” Naye Samweli akaamka, kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Eli akasema, “Mwanangu, sikukuita, rudi ukalale.”

7 Wakati huu Samweli alikuwa bado hajamjuaBwana. Neno laBwanalilikuwa bado halijafunuliwa kwake.

8 Bwanaakamwita Samweli mara ya tatu, naye Samweli akaamka kwenda kwa Eli na kusema, “Mimi hapa, kwa kuwa umeniita.”

Ndipo Eli akatambua kuwaBwanaalikuwa akimwita kijana.

9 Hivyo Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale, na kama akikuita, sema, ‘NenaBwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.’ ” Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake.

10 Bwanaakaja akasimama hapo, akiita kama mara zile nyingine, “Samweli! Samweli!”

Kisha Samweli akasema, “NenaBwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiliza.”

11 NayeBwanaakamwambia Samweli: “Tazama, nipo karibu kufanya kitu katika Israeli ambacho kitafanya masikio ya kila mmoja atakayesikia yawashe.

12 Wakati huo nitatimiza dhidi ya Eli kila kitu nilichonena dhidi ya jamaa yake, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

13 Kwa kuwa nilimwambia kwamba ningehukumu jamaa yake milele kwa sababu ya dhambi aliyoijua, wanawe kumkufuru Mungu, naye akashindwa kuwazuia.

14 Kwa hiyo, nikaapa kuhusu nyumba ya Eli, ‘Hatia ya nyumba ya Eli kamwe haitaweza kufidiwa kwa dhabihu au sadaka.’ ”

15 Samweli akalala mpaka asubuhi, kisha akafungua milango ya nyumba yaBwana. Aliogopa kumwambia Eli yale maono,

16 lakini Eli akamwita na kumwambia, “Samweli mwanangu.”

Samweli akamjibu, “Mimi hapa.”

17 Eli akamwuliza, “Ni nini alichokuambia? Usinifiche.Bwanana ashughulike nawe, tena kwa ukali, kama utanificha cho chote alichokuambia.”

18 Kwa hiyo Samweli akamwambia kila kitu, bila kumficha cho chote. Ndipo Eli akasema, “Yeye niBwana; na afanye lile lililo jema machoni pake!”

19 Bwanaalikuwa pamoja na Samweli alipokuwa akikua, na hakuacha hata moja ya maneno yake lianguke chini.

20 Nao Israeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba wakatambua kuwa Samweli amethibitishwa kuwa nabii waBwana.

21 Bwanaakaendelea kutokea huko Shilo, na huko kujidhihirisha kwa Samweli kwa njia ya neno lake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1SA/3-361bf88a206e6f8392e895de002b749f.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nineteen − one =