1 Wafalme 19

Eliya Akimbilia Horebu

1 Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.

2 Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.”

3 Eliya aliogopa, na akakimbia kuokoa maisha yake. Alipofika Beer-Sheba katika Yuda, akamwacha mtumishi wake huko,

4 lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa,Bwana, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.”

5 Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.

Mara malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka na ule.”

6 Akatazama pande zote, napo hapo karibu na kichwa chake palikuwepo mkate uliookwa kwenye makaa ya moto na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.

7 Yule malaika waBwanaakaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.”

8 Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini mchana na usiku mpaka akafika Horebu, mlima wa Mungu.

9 Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule.

Bwana Amtokea Eliya

Nalo neno laBwanalikamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Eliya?”

10 Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili yaBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wanaitafuta roho yangu waitoe pia.”

11 Bwanaakasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele zaBwana, kwa kuwaBwanayu karibu kupita hapo.”

Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele zaBwana, lakiniBwanahakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakiniBwanahakuwamo kwenye lile tetemeko.

12 Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakiniBwanahakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona.

13 Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mdomo wa pango.

Kisha ile sauti ikamwambia, “Eliya, unafanya nini hapa?”

14 Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili yaBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamekataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao wanaitafuta roho yangu waitoe.”

15 Bwanaakamwambia, “Rudi kwa njia uliyoijia, uende kwenye Jangwa la Dameski. Wakati utakapofika huko, mtie Hazaeli mafuta awe mfalme wa Aramu.

16 Pia mtie mafuta Yehu mwana wa Nimshi awe mfalme wa Israeli, na umtie Elisha mwana wa Shafati kutoka Abel-Mehola mafuta awe nabii badala yako.

17 Yehu atamwua ye yote atakayeutoroka upanga wa Hazaeli, naye Elisha atamwua ye yote atakayeutoroka upanga wa Yehu.

18 Hata sasa nimeweka akiba watu 7,000 katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, nao wote ambao midomo yao haijambusu.”

Wito Wa Elisha

19 Hivyo Eliya akaondoka kutoka huko na kumkuta Elisha mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliongoza ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akamrushia vazi lake.

20 Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.”

Eliya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekutendea nini?.”

21 Basi Elisha akamwacha Eliya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Eliya, akamtumikia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/19-4f7b4d84c5c60d75b3908c03b0c643e4.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 + seven =