2 Mambo ya nyakati 19

Mwonaji Yehu Amkemea Yehoshafati

1 Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu.

2 Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukiaBwana? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu yaBwanaiko juu yako.

3 Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.”

Yehoshafati Aweka Waamuzi

4 Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza watu wakamrudiaBwana, Mungu wa baba zao.

5 Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma.

6 Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili yaBwanaambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu.

7 Basi sasa hofu yaBwanana iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwaBwanaMungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo wala rushwa.”

8 Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili yaBwanana kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.

9 Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho chaBwana.

10 Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasitende dhambi dhidi yaBwana, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.

11 “Amaria Kuhani Mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lo lote linalomhusuBwananaye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kuhusiana na jambo lo lote la mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, nayeBwanaatakuwa pamoja na wale watendao vyema.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/19-738292e7d347d9b4cb4a35538b39fdae.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 + 7 =