2 Mambo ya nyakati 7

Hekalu Lawekwa Wakfu

1 Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu waBwanaukalijaza Hekalu.

2 Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu laBwanakwa sababu utukufu waBwanaulilijaza.

3 Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu waBwanaukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuruBwanawakisema,

“Yeye ni mwema;

upendo wake unadumu milele.”

4 Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele zaBwanaMungu.

5 Naye Mfalme Solomoni akatoa dhabihu ya ng’ombe 22,000 pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu.

6 Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vyaBwanaambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifuBwana, navyo vilitumika wakati aliposhukuru, akisema, “Upendo wake wadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.

7 Solomoni akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu laBwanana huko ndiko akatolea sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka na za mafuta.

8 Kwa hiyo Mfalme Solomoni akaadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, akiwa pamoja na Israeli wote, kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Wadi ya Misri.

9 Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba zaidi.

10 Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Solomoni akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingiBwanaMungu aliomtendea Daudi na Solomoni na kwa ajili ya watu wake Israeli.

Bwana Mungu Amtokea Solomoni

11 Solomoni alipokuwa amemaliza kujenga Hekalu laBwanana jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu laBwanana katika jumba lake mwenyewe la kifalme,

12 BwanaMungu akamtokea Solomoni usiku na kumwambia:

“Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu.

13 “Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu,

14 kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.

15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa.

16 Kwa maana sasa nimechagua na kutakasa Hekalu hili ili kwamba Jina langu lipate kuwa huko milele. Macho yangu na moyo wangu utakuwepo huko daima.

17 “Kwa habari yako wewe, kama ukienenda mbele zangu kama Daudi baba yako alivyoenenda na kufanya yote nikuamuruyo, nawe ukizishika amri zangu na sheria zangu,

18 Nitakifanya imara kiti chako cha enzi kama nilivyoagana na Daudi baba yako wakati niliposema, ‘Hutakosa kamwe mtu wa kutawala juu ya Israeli.’

19 “Lakini kama ukigeuka na kuyaacha maagizo na amri nilizowapa na kwenda kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,

20 ndipo nitakapoing’oa Israeli kutoka katika nchi yangu niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Nitalifanya kitu cha kudharauliwa na kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa mataifa yote.

21 Ingawa Hekalu hili sasa ni la fahari sana, wale wote watakaopita watashangaa na kusema, ‘Kwa niniBwanaamefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’

22 Watu watajibu, ‘Ni kwa sababu wamemwachaBwana, Mungu wa baba zao, ambaye aliwatoa Misri, nao wamekumbatia miungu mingine, wakaiabudu na kuitumikia, hiyo ndiyo sababu alileta haya maafa yote juu yao.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/7-09cfd4e173b5ffc8dda972df8e82b579.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen − 13 =