Hagai 1

Wito Wa Kuijenga Nyumba Ya Bwana

1 Katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario wa Uajemi, katika siku ya kwanza ya mwezi wa sita, neno laBwanalilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda na kwa Kuhani Mkuu Yoshuamwana wa Yehosadaki:

2 Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: “Hawa watu husema, ‘Wakati haujawadia wa kujenga nyumba yaBwana.’ ”

3 Kisha neno laBwanalikaja kupitia kwa nabii Hagai:

4 “Je, ni wakati wenu ninyi wa kuishi katika nyumba zenu zilizojengwa vizuri, wakati hii nyumba ikibaki, gofu?”

5 Sasa hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.

6 Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.”

7 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.

8 Pandeni milimani mkalete miti na kujenga nyumba, ili nipate kuifurahia nitukuzwe.”

9 “Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe.

10 Kwa hiyo, kwa sababu yenu mbingu zimezuia umande wake na ardhi mavuno yake.

11 Niliita ukame mashambani na milimani, kwenye nafaka, mvinyo mpya, mafuta pamoja na cho chote kinachozalishwa na ardhi, juu ya watu na ng’ombe, pamoja na kazi za mikono yenu.”

12 Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua Kuhani Mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti yaBwanaMungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa naBwanaMungu wao. Watu walimwogopaBwana.

13 Kisha Hagai, mjumbe waBwana, akawapa watu ujumbe huu waBwana, “Mimi niko pamoja nanyi,” asemaBwana.

14 Kwa hiyoBwanaakachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Kuhani Mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho ya mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wao,

15 katika siku ya ishirini na nne mwezi wa sita katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/HAG/1-69a75d53ced7552db5a3c2fe4a8597fc.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

15 − 12 =