Hesabu 28

Sadaka Za Kila Siku

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’

3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtoleaBwana: wana kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.

4 Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni,

5 kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efaya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hiniya mafuta ya zeituni.

6 Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

7 Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwaBwanamahali patakatifu.

8 Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

Sadaka Za Sabato

9 “ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efaza unga laini uliochanganywa na mafuta.

10 Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.

Sadaka Za Kila Mwezi

11 “ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamleteaBwanasadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.

12 Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efauliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta;

13 pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwaBwana.

14 Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hiniya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini; na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka.

15 Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwaBwanakama sadaka ya dhambi.

Pasaka

16 “ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza itafanyika Pasaka yaBwana.

17 Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mkate usiotiwa chachu.

18 Katika siku ya kwanza mwe na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida.

19 Leteni mbele zaBwanasadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo waume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

20 Pamoja na kila fahali andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa;

21 pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa.

22 Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu.

23 Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi.

24 Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayoBwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

25 Siku ya saba muwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kaiwada.

Sikukuu Ya Majuma

26 “ ‘Siku ya malimbuko, mnapomleteaBwanasadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi za kawaida.

27 Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

28 Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini;

29 na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba.

30 Ongeza Beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

31 Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/28-c47f33263bb0d321271ec9fcdcc0debe.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 + fifteen =