Hesabu 3

Walawi

1 Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati uleBwanaalipozungumza na Mose, katika Mlima Sinai.

2 Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.

3 Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, ambao walikuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.

4 Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele zaBwanawakati walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari peke yao walihudumu kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.

5 Bwanaakamwambia Mose,

6 “Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.

7 Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.

8 Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.

9 Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kabisa kwake.

10 Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine ye yote atakayesogelea mahali patakatifu ni lazima auawe.”

11 Bwanaakamwambia Mose,

12 “Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,

13 kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimiBwana.”

14 Bwanaakamwambia Mose katika Jangwa la Sinai,

15 “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

16 Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno laBwana.

17 Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi:

Gershoni, Kohathi na Merari.

18 Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagerishoni:

Libni na Shimei.

19 Koo za Wakohathi zilikuwa ni:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

20 Koo za Wamerari zilikuwa ni:

Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

21 Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagerishoni.

22 Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500.

23 Ukoo wa Wagerishoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.

24 Kiongozi wa jamaa za Wagerishoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.

25 Katika Hema la Kukutania, Wagerishoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,

26 mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

27 Kwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamrami, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi.

28 Hesabu ya wanaume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.

29 Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.

30 Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.

31 Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.

32 Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

33 Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari.

34 Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200.

35 Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.

36 Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,

37 na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

38 Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea maawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine ye yote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.

39 Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri yaBwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mwanaume mwenye mwezi mmoja au zaidi walikuwa 22,000.

40 Bwanaakamwambia Mose, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao.

41 Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimiBwana.”

42 Hivyo Mose akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kamaBwanaalivyomwamuru.

43 Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza waume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina walikuwa 22,273.

44 Bwanaakamwambia Mose,

45 “Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimiBwana.

46 Ili kukomboa wazao wa kwanza 273 wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi,

47 kusanya shekeli tanokwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.

48 Mpe Aroni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”

49 Kwa hiyo Mose akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi.

50 Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli 1,365kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu.

51 Mose akampa Aroni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamuriwa na neno laBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/3-e86f3cb2b11f7d6ad28c7b04ad5715bb.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

9 + 15 =