Hesabu 31

Kulipiza Kisasi Juu Ya Wamidiani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”

3 Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi chaBwana.

4 Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.”

5 Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli.

6 Mose aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.

7 Walipigana dhidi ya Wamidiani, kamaBwanaalivyomwagiza Mose, nao waliua kila mwanaume.

8 Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vile vile walimwua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga.

9 Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ng’ombe, kondoo na mali zao kama nyara.

10 Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote.

11 Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama,

12 nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ng’ambo ya Yeriko.

13 Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.

14 Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.

15 Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?”

16 “Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasiBwanakwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu waBwana.

17 Sasa waue wavulana wote. Pia umuue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,

18 lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.

19 “Ninyi nyote ambao mmeua mtu ye yote au kumgusa mtu ye yote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.

20 Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”

21 Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari ambao walikuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayoBwanaalimpa Mose:

22 Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,

23 na kitu kingine cho chote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu cho chote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.

24 Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”

Kugawanya Mateka

25 Bwanaakamwambia Mose,

26 “Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.

27 Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.

28 Kutoka katika fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili yaBwanakitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo au mbuzi.

29 Chukua ushuru huu kutoka katika fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu yaBwana.

30 Kutoka katika fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani yaBwana.”

31 Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

32 Nyara zilizobaki kutoka katika mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,

33 ng’ombe 72,000,

34 punda 61,000,

35 na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.

36 Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa:

Kondoo 337,500

37 ambayo ushuru kwa ajili yaBwanailikuwa kondoo 675;

38 ng’ombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa ng’ombe 72;

39 punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa punda 61;

40 Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa watu 32.

41 Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu yaBwana, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

42 Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,

43 nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,

44 ng’ombe 36,000,

45 punda 30,500,

46 na wanadamu 16,000.

47 Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kamaBwanaalivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani yaBwana.

48 Kisha maafisa ambao walikuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose

49 na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana.

50 Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwaBwanavyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele zaBwana.”

51 Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakishiwa.

52 Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimleteaBwanakama zawadi ilikuwa shekeli 16,750.

53 Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi.

54 Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele zaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/31-eadb759677f6f7a0016d2908c1fe3554.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen + sixteen =