Isaya 30

Ole Wa Taifa Kaidi

1 Bwanaasema,

“Ole wa watoto wakaidi,

kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,

wakifanya umoja, lakini si kwa Roho wangu,

wakilundika dhambi juu ya dhambi,

2 wale washukao kwenda Misri

bila kutaka shauri langu,

wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,

watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

3 Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,

kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

4 Ingawa wana maafisa katika Soani

na wajumbe wamewasili katika Hanesi,

5 kila mmoja ataaibishwa

kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,

ambalo haliwaletei msaada wala faida,

bali aibu tu na fedheha.”

6 Neno kuhusu wanyama wa Negebu:

Katika nchi ya taabu na shida,

ya simba waume na wake,

ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao,

wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda,

hazina zao juu ya nundu za ngamia,

kwa lile taifa lisilokuwa na faida,

7 kuvipeleka Misri,

ambaye msaada wake haufai kabisa.

Kwa hiyo nimemwita “Rahabu, yaani, yeye aketiye

kimya bila kufanya cho chote.”

8 Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,

liandike kwenye kitabu,

ili kwa ajili ya siku zijazo

liweze kuwa shahidi milele.

9 Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,

watoto ambao hawataki

kusikiliza mafundisho yaBwana.

10 Wanawaambia waonaji,

“Msione maono tena!”

Nako kwa manabii wanasema,

“Msiendelee kutupatia maono

ambayo ni ya kweli!

Tuambieni mambo ya kupendeza,

tabirini mambo ya uongo.

11 Acheni njia hii,

ondokeni katika mapito haya,

nanyi acheni kutukabili pamoja

na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”

12 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,

mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu,

13 dhambi hii itakuwa kwenu

kama ukuta mrefu,

wenye ufa na wenye kubetuka,

ambao unaanguka ghafula,

kwa mara moja.

14 Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo

ukipasuka pasipo huruma

ambapo katika vipande vyake

hakuna kipande kitakachopatikana

kwa kuukulia makaa kutoka mekoni

au kuchotea maji kisimani.”

15 Hili ndiloBwanaMwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:

“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,

katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,

lakini hamkutaka.

16 Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’

Kwa hiyo mtakimbia!

Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’

Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi!

17 Watu 1,000 watakimbia

kwa ajili ya kitisho cha mtu mmoja,

kwa vitishio vya watu watano

wote mtakimbia,

hadi mtakapoachwa

kama mlingoti wa bendera

juu ya kilele cha mlima,

kama bendera juu ya kilima.”

18 Hata hivyoBwanaanatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwaBwanani Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

19 Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazama jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu.

20 Ingawa Bwana huwapa chakula cha shida na maji ya taabu, walimu wenu hawatafichwa tena, kwa macho yenu wenyewe mtawaona.

21 Kwamba mtageuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu, ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.”

22 Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu, mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”

23 Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana tena kwa wingi. Katika siku ile ng’ombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.

24 Maksai na punda walimao watakula majani makavu na vyakula vilivyotengenezwa, vinavyotandazwa kwa uma na sepeto.

25 Katika siku ile ya mauaji makuu, wakati minara itakapoanguka, vijito vya maji vitatiririka juu ya kila milima mirefu na kila kilima kilichoinuka sana.

26 Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang’aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakatiBwanaatakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.

27 Tazama, hilo Jina laBwanalinakuja kutoka mbali,

likiwa na hasira kali inayowaka

pamoja na wingu zito la moshi,

midomo yake imejaa ghadhabu

na ulimi wake ni moto ulao.

28 Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,

yakipanda hadi shingoni.

Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,

huweka lijamu katika mataya ya mataifa

ambayo huwaongoza upotevuni.

29 Nanyi mtaimba kama usiku mnaoadhimisha

sikukuu takatifu,

mioyo yenu itashangilia

kama vile watu wanapokwea na filimbi

kwenye mlima waBwana,

kwa Mwamba wa Israeli.

30 Bwanaatawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,

naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka

pamoja na hasira yake kali na moto ulao,

kukiwa na tufani ya mvua,

ngurumo za radi na mvua ya mawe.

31 Sauti yaBwanaitaivunjavunja Ashuru,

kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.

32 Kila pigoBwanaatakaloliweka juu yao

kwa fimbo yake ya kuadhibu,

litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,

anapopigana nao katika vita

kwa mapigo ya mkono wake.

33 Tofethi imeandaliwa toka zamani,

imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.

Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu

na kwa upana mkubwa,

likiwa na moto na kuni tele;

pumzi yaBwana,

kama kijito cha kiberiti,

huuwasha moto.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/30-0fdc42da734d063b43738287f9512bc2.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 + seventeen =