Kumbukumbu La Torati 14

Vyakula Vilivyo Najisi Na Vilivyo Safi

1 Ninyi ni watoto waBwanaMungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa,

2 kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwaBwanaMungu wenu.Bwanaamewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.

3 Msile kitu cho chote ambacho ni machukizo.

4 Hawa ndio wanyama mtakaokula: ng’ombe, kondoo, mbuzi,

5 kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani.

6 Mnaweza kumla mnyama ye yote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua.

7 Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.

8 Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

9 Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula ye yote aliye na mapezi pamoja na magamba.

10 Lakini cho chote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

11 Mnaweza kula ndege ye yote aliye safi.

12 Lakini wafuatao msiwale: tai, kipungu, kipungu mweusi,

13 kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yo yote,

14 kunguru wa aina yo yote,

15 mbuni, kirukanjia, dudumizi, kipanga wa aina yo yote

16 bundi, muvurila, bundi mkubwa,

17 mwari, nderi, ndezi, mnandi,

18 membe, koikoi wa aina yo yote, hudihudi na popo.

19 Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.

20 Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

21 Msile kitu cho chote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni ye yote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwaBwanaMungu wenu.

Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Zaka

22 Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka.

23 Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo na mbuzi mbele zaBwanaMungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimuBwanaMungu wenu daima.

24 Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa naBwanaMungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali paleBwanaatakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),

25 basi badilisheni zaka yenu kuwa fedha, mkaichukue hiyo fedha mwende nayo mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua.

26 Tumieni hiyo fedha kununua cho chote ukitakacho: ng’ombe, kondoo, divai au kinywaji cho chote chenye chachu au cho chote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele zaBwanaMungu wenu na kufurahi.

27 Msiache kuwajali Walawi waishio katika miji yenu, kwa kuwa hao hawana shamba wala urithi wao wenyewe.

28 Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu,

29 ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, iliBwanaMungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/14-3ccbf53850fb3f6d71aa3430deb33540.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

9 + 15 =