Kumbukumbu La Torati 16

Pasaka

1 Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka yaBwanaMungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.

2 Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwaBwanaMungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng’ombe, mahali pale ambapoBwanaatapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.

3 Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa hamira, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri.

4 Hamira isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yo yote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.

5 Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wo wote ambaoBwanaMungu wenu amewapa,

6 isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri.

7 Okeni na mle mahali pale ambapoBwanaMungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu.

8 Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili yaBwanaMungu wenu na msifanye kazi.

Sikukuu Ya Mavuno

9 Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka.

10 Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwaBwanaMungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayoBwanaMungu wenu amewapa.

11 Shangilieni mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.

12 Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.

Sikukuu Ya Vibanda

13 Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu.

14 Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu.

15 Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu yaBwanaMungu wenu katika mahali atakapopachaguaBwana. Kwa kuwaBwanaMungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.

16 Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele zaBwanamikono mitupu:

17 Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyoBwanaMungu wenu alivyowabariki.

Waamuzi

18 Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambaoBwanaMungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa.

19 Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki.

20 Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa.

Kuabudu Miungu Mingine

21 Msisimamishe nguzo yo yote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengeaBwanaMungu wenu,

22 wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maanaBwanaMungu wenu anavichukia vitu hivi.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/16-d4f6f98e5664fa92f4ef6cd7f524d45f.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seven + 2 =