Kumbukumbu La Torati 18

Sadaka Kwa Makuhani Na Walawi

1 Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili yaBwanaza kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao.

2 Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao;Bwanandiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

3 Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo.

4 Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu,

5 kwa kuwaBwanaMungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina laBwanasiku zote.

6 Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapoBwanaatapachagua,

7 anaweza akahudumu katika jina laBwanaMungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele zaBwana.

8 Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.

Matendo Ya Machukizo

9 Wakati mtakapoingia katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

10 Asionekane mtu ye yote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi,

11 wala alogaye kwa kupiga mafundo, wala apandishaye pepo, anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

12 Mtu ye yote afanyaye mambo haya ni chukizo kwaBwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maanaBwanaMungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.

13 Kamwe msilaumiwe mbele zaBwanaMungu wenu.

Nabii

14 Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi,BwanaMungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo.

15 BwanaMungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Lazima mumsikilize yeye.

16 Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwombaBwanaMungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti yaBwanaMungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”

17 Bwanaakaniambia: “Wanachosema ni vyema.

18 Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru.

19 Kama mtu ye yote hakusikiliza maneno yangu ambayo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha.

20 Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu cho chote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”

21 Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa naBwana?”

22 Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina laBwanahakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambaoBwanahakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/18-c2b66949ba184d38da65476c92845154.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

20 + 7 =