Kumbukumbu La Torati 23

Kutengwa Na Mkutano

1 Asiingie mtu ye yote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko laBwana.

2 Mtu ye yote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko laBwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

3 Hapatakuwa na Mwamori au Mmoabi au ye yote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko laBwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

4 Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimuili kuwalaani ninyi.

5 Hata hivyo,BwanaMungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababuBwanaMungu wenu anawapenda.

6 Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

7 Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake.

8 Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko laBwana.

Unajisi Katika Kambi

9 Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu cho chote kisicho safi.

10 Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko.

11 Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

12 Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.

13 Kama sehemu ya vifaa vyenu iweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.

14 Kwa kuwaBwanaMungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu cho chote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

Sheria Mbalimbali

15 Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

16 Mwache aishi miongoni mwenu mahali po pote anapopapenda na katika mji wo wote anaochagua. Usimwonee.

17 Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

18 Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba yaBwanaMungu wako kwa ajili ya nadhiri yo yote, kwa sababuBwanaMungu wako anachukizwa na yote mawili.

19 Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine cho chote ambacho waweza kupata riba juu yake.

20 Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwambaBwanaMungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoiingia kuimiliki.

21 Ukiweka nadhiri kwaBwanaMungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwaBwanaMungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

22 Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia.

23 Cho chote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele zaBwanaMungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

24 Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke cho chote kwenye kikapu chako.

25 Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/23-53383c563ac1f5e66e79b39871b3173e.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 1 =