Kumbukumbu La Torati 30

Mafanikio Baada Ya Kumgeukia Bwana

1 Wakati baraka hizi zote pamoja na laana nilizoziweka mbele yako zitakapokujia, nawe ukazitafakari moyoni popoteBwanaMungu wako atakapokutawanya miongoni mwa mataifa,

2 hapo wewe na watoto wako mtakapomrudiaBwanaMungu wako, na kumtii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote kulingana na kila kitu ninachokuamuru leo,

3 ndipoBwanaMungu wako atakapokurudisha kutoka utumwani na kukuhurumia, naye atakukusanya tena kutoka katika mataifa yote kule alikokutawanya wewe.

4 Hata kama umefukuziwa katika nchi ya mbali kiasi gani chini ya mbingu, kutoka hukoBwanaMungu wako atakukusanya na kukurudisha.

5 Atakurudisha katika nchi iliyokuwa mali ya baba zako, nawe utaimiliki. Atakufanya ufanikiwe sana na kukuzidisha kwa idadi kuliko baba zako.

6 BwanaMungu wako ataitairi mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi.

7 BwanaMungu wako ataweka laana hizi zote juu ya adui zako ambao wanakuchukia na kukutesa.

8 Utamtii tenaBwanana kuzishika amri zake zote ninazokupa leo.

9 NdipoBwanaMungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako.Bwanaatakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako,

10 kama ukimtiiBwanaMungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukiaBwanaMungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.

Uzima Na Mauti

11 Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza.

12 Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?”

13 Wala hakiko ng’ambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?”

14 La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.

15 Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo.

16 Ninakuamuru leo kwamba umpendeBwanaMungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, nayeBwanaMungu wako atakubariki katika nchi unayoiingia kuimiliki.

17 Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu,

18 nakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

19 Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi,

20 na ili upate kumpendaBwanaMungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwaBwanandiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaki na Yakobo.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/30-7e4558bdab08c84d5d0739a04ab37b77.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × three =