Kutoka 7

1 KishaBwanaakamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako.

2 Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Aroni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake.

3 Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hata ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri,

4 hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka mkono wangu juu ya Misri, na kwa matendo makuu ya hukumu nitavitoa vikundi vyangu, watu wangu Waisraeli.

5 Nao Wamisri watajua kuwa Mimi ndimiBwananitakapounyosha mkono wangu dhidi ya Misri na kuwatoa Waisraeli watoke humo.”

6 Mose na Aroni wakafanya sawasawa kama vileBwanaalivyowaagiza.

7 Mose alikuwa na umri wa miaka themanini na Aroni alikuwa na umri wa miaka themanini na mitatu walipozungumza na Farao.

Fimbo Ya Aroni Yawa Nyoka

8 Bwanaakamwambia Mose na Aroni,

9 “Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni mwujiza,’ basi mwambie Aroni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.”

10 Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vileBwanaalivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka.

11 Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao.

12 Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao.

13 Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vileBwanaalivyokuwa amesema.

Pigo La Kwanza: Damu

14 KishaBwanaakamwambia Mose, “Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwaachia watu kuondoka.

15 Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ungoje ukingoni mwa Nile ili kuonana naye, nawe uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka.

16 Kisha umwambie, ‘Bwana, Mungu wa Waebrania, amenituma nikuambie: Uwaachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu jangwani. Lakini hadi sasa hujasikiliza.

17 Hili ndiloBwanaasemalo: Kwa hili utajua kuwa Mimi ndimiBwana: Fimbo iliyo mkononi mwangu nitapiga nayo maji ya Nile nayo yatabadilika kuwa damu.

18 Samaki waliomo katika Mto Nile watakufa, nao mto utanuka vibaya, Wamisri hawataweza kunywa hayo maji yake.’ ”

19 Bwanaakamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Chukua ile fimbo yako unyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya chemchemi na mifereji, juu ya madimbwi na mabwawa yote,’ navyo vitabadilika kuwa damu. Damu itakuwa kila mahali katika Misri, hata kwenye vyombo vya miti na vya mawe.”

20 Mose na Aroni wakafanya kama vileBwanaalivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Nile, na maji yote yakabadilika kuwa damu.

21 Samaki katika Mto Nile wakafa, nao mto ukanuka vibaya sana kiasi kwamba Wamisri hawakuweza kunywa maji yake. Damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri.

22 Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vileBwanaalivyokuwa amesema.

23 Badala yake, akageuka akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni.

24 Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Nile kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto.

Pigo La Pili: Vyura

25 Zilipita siku saba baada yaBwanakuyapiga maji ya Mto Nile.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EXO/7-9fb9d369450f2de775bc9c295e7f62b9.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen + seventeen =