Malaki 1

1 Ujumbe: Neno laBwanakwa Israeli kupitia kwa Malaki.

Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa

2 Bwanaasema, “Nimewapenda ninyi.”

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ”

Bwanaasema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo,

3 lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.”

4 Edomu anaweza kusema, “Ingawa tumepondwapondwa, tutajenga upya magofu.”

Lakini hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: “Wanaweza kujenga, lakini nitabomoa. Wataitwa Nchi Ovu, watu ambao siku zote wapo chini ya ghadhabu yaBwana.

5 Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘Bwanani mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’

Dhabihu Zilizo Na Mawaa

6 “Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Ni ninyi, Enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu.

“Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’

7 “Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu.

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’

“Kwa kusema kuwa meza yaBwanani ya kudharauliwa.

8 Wakati mletapo dhabihu wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahiwa nanyi? Je, atawakubalia?” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

9 “Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

10 “Laiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.

11 Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia maawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Lakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, ‘Imetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.’

13 Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Wakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asemaBwana.

14 “Amelaaniwa yeye adanganyaye aliye na mnyama wa kiume anayekubalika katika kundi lake na kuweka nadhiri ya kumtoa, lakini akatoa dhabihu ya mnyama aliye na dosari kwaBwana. Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langu linapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/1-2d81f459cdbe68056fa3c5106d0e3452.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

7 + fifteen =