Mambo ya Walawi 10

Kifo Cha Nadabu Na Abihu

1 Nadabu na Abihu wana wa Aroni wakachukua vyetezo vyao, wakaweka moto ndani yake na kuongeza uvumba; kisha wakamtoleaBwanamoto usio halali, kinyume na agizo la Mungu.

2 Hivyo moto ukaja kutoka katika uwepo waBwanana kuwaramba, nao wakafa mbele zaBwana.

3 Kisha Mose akamwambia Aroni, “Hili ndilo alilonenaBwanawakati aliposema:

“ ‘Miongoni mwa wale watakaonikaribia

nitajionyesha kuwa mtakatifu;

machoni pa watu wote

nitaheshimiwa.’ ”

Aroni akanyamaza.

4 Mose akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjomba wake Aroni, akawaambia, “Njoni hapa; itoeni miili ya binamu zenu nje ya kambi mbali na mahali patakatifu.”

5 Hivyo wakaja na kuwaondoa, wakiwa wamevalia makoti yao ya ibada, wakawapeleka nje ya kambi, kama Mose alivyoamuru.

6 Ndipo Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe, Eleazari na Ithamari, “Msifunue vichwa vyenu wala msirarue mavazi yenu, la sivyo mtakufa naBwanaataikasirikia jumuiya nzima. Lakini ndugu zenu, nyumba yote ya Israeli wanaweza kuwaombolezea wale ambaoBwanaamewaangamiza kwa moto.

7 Msitoke nje ya ingilio la Hema la Kukutania la sivyo mtakufa, kwa sababu mafuta yaBwanaya upako yako juu yenu.” Kwa hiyo wakafanya kama vile Mose alivyosema.

8 KishaBwanaakamwambia Aroni,

9 “Wewe na wanao msinywe mvinyo wala kinywaji kingine kilichochachuka wakati mwingiapo katika Hema la Kukutania, la sivyo mtakufa. Hili litakuwa Agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.

10 Ni lazima mtenganishe kilicho kitakatifu na kile kilicho cha kawaida, kati ya yaliyo najisi na yaliyo safi,

11 na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazoBwanaaliwapa kupitia Mose.”

12 Mose akamwambia Aroni pamoja na wanawe waliosalia, Eleazari na Ithamari, “Chukueni sadaka ya nafaka iliyobaki kutoka katika sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto, muile hapo kando ya madhabahu ikiwa imeandaliwa bila chachu, kwa sababu ni takatifu sana.

13 Mtaila katika mahali patakatifu kwa sababu ni fungu lenu na fungu la wana wenu la sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto, kwa maana hivyo ndivyo nilivyoamuriwa.

14 Lakini wewe na wanao na binti zako mwaweza kula kidari kile kilichoinuliwa na paja lile lililotolewa. Mtavila mahali safi pa kawaida ya ibada; mmepewa wewe na watoto wako kuwa fungu lenu la sadaka za amani za Waisraeli.

15 Paja lile lililotolewa na kidari kile kilichoinuliwa lazima viletwe pamoja na sehemu za mafuta ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, ili kuinuliwa mbele zaBwanakama sadaka ya kuinuliwa. Hili litakuwa fungu lako la kawaida na wanao, kamaBwanaalivyoagiza.”

16 Mose alipouliza kuhusu mbuzi atolewaye kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na kukuta kwamba ameteketezwa, aliwakasirikia Eleazari na Ithamari, wana wa Aroni waliobaki, akawauliza,

17 “Kwa nini hamkula sadaka ya dhambi katika eneo la mahali patakatifu? Ni takatifu sana, mlipewa ninyi ili kuondoa hatia ya jumuiya kwa ajili ya kuwafanyia upatanisho mbele zaBwana.

18 Kwa kuwa damu yake haikuletwa ndani ya Mahali Patakatifu, mngemla mbuzi huyo ndani ya mahali patakatifu kama nilivyoagiza.”

19 Aroni akamjibu Mose, “Leo wanangu wametoa sadaka zao za dhambi na sadaka zao za kuteketezwa mbele zaBwana, lakini mambo kama haya yamenitokea mimi. Je,Bwanaangependezwa kama ningekuwa nimekula sadaka ya dhambi leo?”

20 Mose aliposikia haya, akaridhika.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/10-8a6f20c18b66629902eb1ed084ce8489.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − ten =