Mambo ya Walawi 19

Sheria Mbalimbali

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: ‘Iweni watakatifu kwa sababu Mimi,BwanaMungu wenu, ni mtakatifu.

3 “ ‘Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

4 “ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.

5 “ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwaBwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.

6 Sadaka hiyo italiwa siku iyo hiyo mnayoitoa au kesho yake; cho chote kitakachobaki hadi siku ya tatu lazima kiteketezwe kwa moto.

7 Kama sehemu yo yote ya sadaka hiyo italiwa siku ya tatu, itakuwa si safi nayo haitakubaliwa.

8 Ye yote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwaBwana; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.

9 “ ‘Wakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako.

10 Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

11 “ ‘Usiibe.

“ ‘Usiseme uongo.

“ ‘Msidanganyane.

12 “ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

13 “ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako.

“ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

14 “ ‘Usimlaani kiziwi wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

15 “ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

16 “ ‘Usiende huko na huko ukieneza uchochezi miongoni mwa watu wako.

“ ‘Usifanye kitu cho chote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimiBwana.

17 “ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.

18 “ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimiBwana.

19 “ ‘Mtazishika amri zangu.

“ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti.

“ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako.

“ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti.

20 “ ‘Kama mwanaume atakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru.

21 Hata hivyo huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwaBwana.

22 Pamoja na kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele zaBwanakwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

23 “ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yo yote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa.

24 Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwaBwana.

25 Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezwa. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

26 “ ‘Msile nyama yo yote yenye damu ndani yake.

“ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.

27 “ ‘Nywele za kichwa zisikatwe denge wala kunyoa pembe za ndevu zenu.

28 “ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimiBwana.

29 “ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.

30 “ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimiBwana.

31 “ ‘Msiwaendee waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

32 “ ‘Uwapo mbele ya mzee usimame, kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimiBwana.

33 “ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.

34 Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimiBwanaMungu wako.

35 “ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi.

36 Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efahalali, na hinihalali. Mimi ndimiBwanaMungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

37 “ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimiBwana.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/19-db6d14733c06153bac2213d6d778dcdc.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five + 15 =