Mambo ya Walawi 2

Sadaka Ya Nafaka

1 “ ‘Mtu ye yote aletapo sadaka ya nafaka kwaBwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake

2 naye atapeleka kwa makuhani wana wa Aroni. Kuhani atachukua konzi moja iliyojaa unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote na kuuteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

3 Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe, ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

4 “ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu na iliyopakwa mafuta.

5 Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta na bila chachu.

6 Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka.

7 Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta.

8 Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwaBwana; mkabidhi kuhani ambaye ataipeleka madhabahuni.

9 Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

10 Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana ya sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

11 “ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwaBwanani lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yo yote au asali katika sadaka itolewayo kwaBwanakwa moto.

12 Unaweza kuzileta kwaBwanakama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza.

13 Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.

14 “ ‘Kama ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwaBwana, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto.

15 Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka.

16 Kuhani atateketeza ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka iliyopondwa kwa mafuta, pamoja na uvumba wote, kama sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/2-24e32029302d8f3709ba31dc1ce6c159.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − 10 =