Mambo ya Walawi 24

Mafuta Na Mikate Mbele Za Bwana

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi yaliyokamuliwa ya zeituni kwa ajili ya mwanga ili kwamba taa ziwe zinawaka mfululizo.

3 Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele zaBwanakuanzia jioni hadi asubuhi kwa mfululizo. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.

4 Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele zaBwanalazima zihudumiwe mfululizo.

5 “Chukua unga laini na uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efaza unga kwa kila mkate.

6 Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele zaBwanajuu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.

7 Kando ya kila mstari weka uvumba safi kama sehemu ya ukumbusho ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.

8 Mikate hii itawekwa mbele zaBwanakila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu.

9 Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.”

Mwenye Kukufuru Apigwa Mawe

10 Basi mwana wa mama wa Kiisraeli ambaye baba yake ni Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli na mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.

11 Huyu mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru Jina laBwanana kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri wa kabila la Dani.)

12 Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi yaBwanayatakapokuwa wazi kwao.

13 NdipoBwanaakamwambia Mose:

14 “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.

15 Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu ye yote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;

16 ye yote atakayekufuru Jina laBwanani lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwapo ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina laBwana, ni lazima auawe.

17 “ ‘Kama mtu ye yote atamwua mtu mwingine, ni lazima auawe.

18 Mtu ye yote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai.

19 Ikiwa mtu ye yote atamjeruhi jirani yake, cho chote alichomtenda naye atatendewa:

20 iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.

21 Ye yote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini ye yote auaye mtu, lazima auawe.

22 Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”

23 Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/24-f8b917f43fb3bf2f920307751a43acfa.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 + eighteen =