Mambo ya Walawi 27

Kukomboa Kile Kilicho Cha Bwana

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Kama mtu ye yote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwaBwana, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana,

3 thamani ya mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini atakombolewa kwa shekeli hamsiniza fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu;

4 ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini.

5 Kama ni mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini, na mwanamke shekeli kumi.

6 Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatuza fedha.

7 Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tanona mwanamke shekeli kumi.

8 Kama mtu ye yote anayeweka nadhiri ni maskini mno kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.

9 “ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwaBwana, mnyama wa namna hiyo aliyetolewa kwaBwanaanakuwa mtakatifu.

10 Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri; kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, huwa watakatifu.

11 Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi kiibada, yaani yule asiye kubalika kuwa sadaka kwaBwana, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani,

12 ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo kama ni mzuri au mbaya. Thamani yo yote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa.

13 Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

14 “ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwaBwana, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo kama ni nzuri au mbaya. Thamani yo yote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa.

15 Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa tena yake.

16 “ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwaBwana, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homerimoja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha.

17 Kama akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa iyo hiyo.

18 Lakini kama akiweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka unaofuata wa Yubile, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa.

19 Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena.

20 Kama pengine halikomboi shamba, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa.

21 Shamba litakapoachiwa mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwaBwana, nalo litakuwa mali ya makuhani.

22 “ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwaBwanashamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake,

23 kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwaBwana.

24 Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake.

25 Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, geraishirini kwa shekeli.

26 “ ‘Kwa vyo vyote, hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali yaBwana; awe maksai au kondoo, ni waBwana.

27 Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

28 “ ‘Lakini cho chote kile mtu alichonacho na kukitoa kwaBwana, ikiwa ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, chaweza kuuzwa au kukombolewa; cho chote kilichotolewa ni kitakatifu sana kwaBwana.

29 “ ‘Mtu ye yote aliyetolewa ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.

30 “ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, ikiwa ni nafaka kutoka kwenye ardhi, au tunda kwenye miti, ni mali yaBwana; ni takatifu kwaBwana.

31 Kama mtu akikomboa cho chote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

32 Zaka yote ya kundi la ng’ombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa mtakatifu kwaBwana.

33 Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”

34 Haya ndiyo maagizoBwanaaliyompa Mose juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/27-2fcd77b31e64f84b296a0b3543b0ef72.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − four =