Mambo ya Walawi 5

Sadaka Nyingine Za Kuondoa Dhambi

1 “ ‘Ikiwa mtu atakuwa ametenda dhambi kwa sababu hakusema alipotakiwa kutoa ushahidi hadharani kuhusu jambo aliloona au kujua habari zake, yeye anastahili adhabu.

2 “ ‘Au kama mtu akigusa kitu cho chote ambacho si safi kwa kawaida ya ibada, kama ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata kama hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.

3 “ ‘Au kama akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu cho chote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata ikiwa hana habari juu yake, atakapojua atakuwa ana hatia.

4 “ ‘Au kama mtu ameapa kufanya kitu cho chote bila kufikiri kikiwa chema au kibaya, kwa vyo vyote mtu aweza kuapa kwa uzembe akiwa hana habari juu yake, hata kama hatambui juu yake kwa vyo vyote, atakapofahamu atakuwa na hatia.

5 “ ‘Wakati mtu ye yote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, lazima akiri kuwa ni kwa njia gani ametenda dhambi,

6 na kwa ajili ya adhabu ya dhambi aliyoitenda lazima alete kwaBwanakondoo jike au mbuzi kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.

7 “ ‘Lakini huyo mtu kama hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwaBwanakuwa adhabu kwa ajili ya dhambi yake, mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa.

8 Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza huyo mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake na kuacha kichwa chake kikining’inia,

9 naye atanyunyiza sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi kwenye pembe za madhabahu, damu iliyobaki lazima ichuruzwe chini ya madhabahu. Hii ni sadaka ya dhambi.

10 Kisha kuhani atamtoa yule wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.

11 “ ‘Ikiwa basi, hawezi kupata hua wawili au makinda mawili ya njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efaya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake kwa sababu ni sadaka ya dhambi.

12 Atauleta kwa kuhani, naye atauchukua unga huo konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.

13 Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi mojawapo ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ”

Sadaka Ya Hatia

14 Bwanaakamwambia Mose:

15 “Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu yaBwana, huyo mtu ataleta kwaBwanakama adhabu, kondoo dume mmoja kutoka katika kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia.

16 Ni lazima alipe kwa yale aliyoshindwa kufanya kuhusu vitu vitakatifu, kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani ile na kuitoa yote kwa kuhani, ambaye atamfanyia upatanisho kwa huyo kondoo dume kama sadaka ya dhambi, naye atasemehewa.

17 “Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri zaBwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.

18 Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa.

19 Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi yaBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/5-af066fdeecbc995d0f06de7814e528c1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × one =