Mambo ya Walawi 7

Sadaka Ya Hatia

1 “ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya hatia, ambayo ni takatifu sana:

2 Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale ambapo sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu.

3 Mafuta yake yote yatatolewa sadaka: mafuta ya mkia na mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani,

4 figo zote mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo yataondolewa pamoja na hizo figo.

5 Kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto. Hii ni sadaka ya hatia.

6 Mwanaume ye yote katika jamaa ya kuhani aweza kuila, lakini lazima iliwe mahali patakatifu, ni takatifu sana.

7 “ ‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawa sawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho.

8 Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya ye yote anaweza kuichukua ile ngozi ya mnyama yule aliyetolewa iwe yake.

9 Kila sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni au kupikwa katika sufuria au katika kikaangio itakuwa ya kuhani anayeitoa

10 na kila sadaka ya nafaka, ikiwa imechanganywa na mafuta au kavu, itakuwa ya wana wa Aroni, nayo itagawanywa sawa.

Sadaka Ya Amani

11 “ ‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya amani ambayo mtu aweza kuileta kwaBwana:

12 “ ‘Ikiwa mtu atatoa sadaka ya amani kwa ajili ya kuonyesha shukrani, ndipo pamoja na sadaka hii ya shukrani, atatoa maandazi yasiyotiwa chachu yaliyochanganywa na mafuta, mikate myembamba isiyotiwa chachu iliyopakwa mafuta, maandazi ya unga laini uliokandwa vizuri na kuchanganywa na mafuta.

13 Pamoja na sadaka hii ya amani ya shukrani ataleta sadaka ya maandazi yaliyotengenezwa kwa chachu.

14 Ataleta moja ya kila aina ya andazi kama sadaka, matoleo kwaBwana; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani.

15 Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu cho chote mpaka asubuhi.

16 “ ‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini cho chote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake.

17 Nyama yo yote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto.

18 Kama nyama yo yote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu,Bwanahataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi, mtu atakayekula sehemu yake yo yote atakuwa na hatia kwa uovu huo.

19 “ ‘Nyama ile inayogusa cho chote ambacho ni najisi kwa kawaida ya ibada kamwe haitaliwa, ni lazima iteketezwe kwa moto. Kuhusu nyama nyingine, mtu ye yote aliye safi kwa kawaida ya ibada anaweza kuila.

20 Lakini kama mtu ye yote ni najisi akila nyama yo yote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwaBwana, huyo mtu atakatiliwa mbali na watu wake.

21 Kama mtu ye yote akigusa kitu kilicho najisi, ikiwa ni uchafu wa mwanadamu, au mnyama najisi, au kitu cho chote kilicho najisi, kitu cha kuchukiza, kisha akala nyama yo yote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwaBwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Kula Mafuta Na Kunywa Damu Kwakatazwa

22 Bwanaakamwambia Mose,

23 “Waambie Waisraeli: ‘Msile mafuta yo yote ya ng’ombe, kondoo wala mbuzi.

24 Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yo yote, lakini kamwe msiyale.

25 Mtu ye yote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwaBwanakwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

26 Po pote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege ye yote wala ya mnyama.

27 Ikiwa mtu ye yote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’ ”

Fungu La Makuhani

28 Bwanaakamwambia Mose,

29 “Waambie Waisraeli: ‘Mtu ye yote aletaye sadaka ya amani kwaBwanaataleta sehemu ya sadaka hiyo kama dhabihu yake kwaBwana.

30 Kwa mikono yake mwenyewe ataileta sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa.

31 Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe.

32 Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo.

33 Mwana wa Aroni atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani, ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake.

34 Kutoka kwenye sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Aroni na wanawe kuwa fungu lao la kawaida kutoka kwa Waisraeli.’ ”

35 Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwaBwanakwa moto ambazo zilitengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu kumtumikiaBwanakatika kazi ya ukuhani.

36 Siku ile walipotiwa mafuta,Bwanaaliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la kawaida kwa vizazi vijavyo.

37 Basi haya ndiyo masharti kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia, sadaka ya kuwekwa wakfu na sadaka ya amani,

38 ambayoBwanaalimpa Mose juu ya mlima Sinai siku ile alipowaagiza Waisraeli walete sadaka zao kwaBwana, katika Jangwa la Sinai.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/7-8d8c1857e4f0a0108791ceceab4492b1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × 5 =