Mika 1

1 Neno laBwanalilimjia Mika, Mmorashti, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.

2 Sikia, Ee mataifa, enyi nyote,

sikilizeni, Ee dunia na wote mliomo ndani yake,

iliBwanaMwenyezi ashuhudie dhidi yenu,

Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.

Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu

3 Tazama!Bwanaanakuja kutoka makao yake;

anashuka na kukanyaga

mahali palipoinuka juu pa dunia.

4 Milima inayeyuka chini yake

na mabonde yanagawanyika

kama nta mbele ya moto,

kama maji yatiririkayo kasi

kwenye mtelemko.

5 Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo,

ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli.

Kosa la Yakobo ni lipi?

Je, sio Samaria?

Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini?

Je, sio Yerusalemu?

6 “Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto,

mahali pa kuotesha mizabibu.

Nitayamwaga mawe yake katika bonde

na kuacha wazi misingi yake.

7 Sanamu zake zote

zitavunjwa vipande vipande;

zawadi zake zote za Hekalu

zitachomwa kwa moto;

nitaharibu vinyago vyake vyote.

Kwa kuwa alikusanya zawadi zake

kutokana na ujira wa kahaba,

nazo zitatumika tena

kulipa mishahara ya kahaba.”

Kulia Na Kuomboleza

8 Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza;

nitatembea bila viatu na tena uchi.

Nitabweka kama mbweha

na kuomboleza kama bundi.

9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki;

limekuja Yuda.

Limefika hasa kwenye lango la watu wangu,

hata Yerusalemu kwenyewe.

10 Usiliseme hili huko Gathi;

usilie hata kidogo.

Huko Beth-le-Afra

ugaegae mavumbini.

11 Piteni mkiwa uchi na wenye aibu,

ninyi mkaao Shafiri.

Wale waishio Saanani

hawatatoka nje.

Beth-Eseli iko katika maombolezo;

kinga yake imeondolewa kwako.

12 Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu

wakingoja msaada,

kwa sababu maangamizi yamekuja

kutoka kwaBwana,

hata katika lango la Yerusalemu.

13 Enyi mkaao Lakishi,

fungeni farasi kwenye magari ya vita.

Mlikuwa chanzo cha dhambi

kwa Binti Sayuni,

kwa kuwa makosa ya Israeli

yalikutwa kwako.

14 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi

zawadi za kuagana.

Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu

kwa wafalme wa Israeli.

15 Nitawaleteeni atakayewashinda

ninyi mnaoishi Maresha.

Yeye aliye utukufu wa Israeli

atakuja Adulamu.

16 Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza

kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia;

jifanyieni upara kama tai,

kwa kuwa watawaacha

na kwenda uhamishoni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MIC/1-c497a0b0b0e802008686ab0250d6b152.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen − 1 =