Mwanzo 10

Mataifa Yaliyotokana Na Noa

1 Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

Wazao Wa Yafethi

2 Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

3 Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

4 Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

5 (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake lenyewe.)

Wazao Wa Hamu

6 Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.

7 Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

8 Kushi alikuwa baba yake Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa mwenye nguvu duniani.

9 Alikuwa mwindaji hodari mbele zaBwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele zaBwana.”

10 Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.

11 Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehobothiri, Kala

12 na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

13 Misraimu alikuwa baba wa:

Waludi, Wanami, Walehabi, Wanaftuhi,

14 Wapathrusi, Wakasluhi (ambao Wafilisti walitokana nao) na Wakaftori.

15 Kanaani alikuwa baba wa:

Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,

16 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

17 Wahivi, Waariki, Wasini,

18 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,

19 na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

20 Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

Wazao Wa Shemu

21 Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

22 Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

23 Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mashi.

24 Arfaksadi alikuwa baba wa Sela,

naye Sela akamzaa Eberi.

25 Eberi akazaa wana wawili:

Mmoja aliitwa Pelegi, kwa kuwa katika wakati wake ndipo dunia ilipogawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

26 Yoktani alikuwa baba wa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

27 Hadoramu, Uzali, Dikla,

28 Obali, Abimaeli, Seba,

29 Ofiri, Havila na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

30 Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

31 Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

32 Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/10-1fd99e32014be110f3e0dad531912a2c.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × 2 =