Mwanzo 12

Wito Wa Abramu

1 Bwanaakawa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.

2 “Mimi nitakufanya taifa kubwa

na nitakubariki,

Nitalikuza jina lako,

nawe utakuwa baraka.

3 Nitawabariki wale wanaokubariki,

na ye yote akulaaniye nitamlaani;

na kupitia kwako mataifa yote duniani

yatabarikiwa.”

4 Hivyo Abramu akaondoka kamaBwanaalivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano.

5 Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.

6 Abramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo.

7 Bwanaakamtokea Abramu akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa Abramu akamjengeaBwanaaliyekuwa amemtokea madhabahu.

8 Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengeaBwanamadhabahu na akaliitia jina laBwana.

9 Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu.

Abramu Katika Nchi Ya Misri

10 Basi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali.

11 Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura.

12 Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai.

13 Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.”

14 Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura.

15 Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akachukuliwa kwenda kwenye jumba lake la kifalme.

16 Kwa ajili ya Sarai, Farao akamtendea Abramu mema, akapata kondoo, ng’ombe, punda, ngamia na watumishi wa kiume na wa kike.

17 LakiniBwanaakamwadhibu Farao na nyumba yake kwa maradhi ya kufisha kwa sababu ya kumchukua Sarai, mke wa Abramu.

18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akamwuliza, “Umenifanyia nini? Kwa nini hukuniambia ni mke wako?

19 Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!”

20 Kisha Farao akawapa watu wake amri kuhusu Abramu, wakamsindikiza pamoja na mke wake na kila alichokuwa nacho.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/12-e048a7de7cef87af73314d799d493030.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 5 =