Mwanzo 15

Agano La Mungu Na Abramu

1 Baada ya jambo hili, neno laBwanalikamjia Abramu katika maono:

“Usiogope, Abramu.

Mimi ni ngao yako,

na thawabu yako kubwa sana.”

2 Lakini Abramu akasema, “EeBwanaMwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?”

3 Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”

4 Ndipo neno laBwanalilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.”

5 Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”

6 Abramu akamwaminiBwana, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.

7 Pia akamwambia, “Mimi ndimiBwana, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.”

8 Lakini Abramu akasema, “EeBwanaMwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?”

9 NdipoBwanaakamwambia, “Niletee mtamba wa ng’ombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.”

10 Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili.

11 Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza.

12 Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake.

13 KishaBwanaakamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao wenyewe, nao watakuwa watumwa na watateswa kwa miaka mia nne.

14 Lakini nitaliadhibu taifa lile wanaolitumikia kama watumwa, hatimaye watatoka huko na mali nyingi.

15 Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema.

16 Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.”

17 Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama.

18 Siku hiyoBwanaakafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia mto wa Misrihadi mto ule mkubwa, Eufrati,

19 yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni,

20 Wahiti, Waperizi, Warefai,

21 Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/15-460d102ba5d44f28ea511a1d317e181d.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 − 4 =