Mwanzo 2

1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.

2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote.

3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Adamu Na Eva

4 Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

BwanaMungu alipoziumba mbingu na dunia,

5 hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwaBwanaMungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi,

6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi:

7 BwanaMungu alimuumba mtu kutoka mavumbiya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, mtu akawa kiumbe hai.

8 BasiBwanaMungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba.

9 BwanaMungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne.

11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu.

12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, lulu na vito shohamu pia hupatikana huko.)

13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi.

14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Eufrati.

15 BwanaMungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza.

16 BwanaMungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wo wote katika bustani,

17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

18 BwanaMungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

19 BasiBwanaMungu alikuwa amefanyiza kutoka katika ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lo lote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake.

20 Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.

21 HivyoBwanaMungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama.

22 KishaBwanaMungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

23 Huyo mwanaume akasema,

“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu

na nyama ya nyama yangu,

# ataitwa ‘mwanamke,’

kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25 Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/2-2d1cbbd845aaad2395f2bf2bd55363d5.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 + five =