Waamuzi 13

Kuzaliwa Kwa Samsoni

1 Waisraeli wakafanya maovu tena mbele zaBwana. HivyoBwanaakawatia mikononi mwa Wafilisti kwa muda wa miaka arobaini.

2 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Sora, aliyeitwa Manoa, wa kabila la Wadani, naye alikuwa na mke ambaye alikuwa tasa na hakuwa na mtoto.

3 Malaika waBwanaakamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na huna mtoto, lakini utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanaume.

4 Lakini ujihadhari sana usinywe mvinyo wala kileo kingine cho chote, wala usile kitu cho chote kilicho najisi,

5 kwa kuwa utachukuwa mimba na utamzaa mtoto mwanaume. Wembe usipite kichwani pake, kwa kuwa huyo mwana atakuwa Mnadhiri wa Mungu, aliyewekwa wakfu kwa ajili ya Mungu tangu tumboni mwa mama yake, naye ataanza kuwakoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti.”

6 Ndipo huyo mwanamke akamwendea mumewe na kumweleza kuwa, “Mtu wa Mungu alinijia. Kule kuonekana kwake kulikuwa kama kwa malaika wa Mungu, wa kutisha sana. Sikumwuliza alikotoka wala hakuniambia jina lake.

7 Lakini aliniambia, ‘Utachukua mimba na utazaa mtoto mwanaume. Basi sasa, usinywe mvinyo wala kileo kingine cho chote wala usile kitu kilicho najisi, kwa kuwa huyo mtoto atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yake mpaka kufa kwake.’ ”

8 Ndipo Manoa akamwombaBwana, akasema: “Ee Bwana, nakusihi, huyo mtu wa Mungu uliyemtuma kwetu aje tena ili atufundishe jinsi ya kumlea huyo mwana atakayezaliwa.”

9 Mungu akamsikia Manoa, naye malaika wa Mungu akamjia tena huyo mwanamke alipokuwa shambani, lakini mumewe Manoa hakuwepo.

10 Basi yule mwanamke akaenda haraka na kumwambia mumewe, “Tazama mtu yule aliyenitokea siku ile yupo hapa!”

11 Manoa akainuka akaandamana na mkewe. Alipomfikia yule mtu akamwuliza, “Je, wewe ndiye yule uliyesema na mke wangu?”

Akasema, “Mimi ndiye.”

12 Basi Manoa akamwuliza “Wakati maneno yako yatakapotimia, masharti ya maisha ya mtoto huyu yatakuwa nini na kazi yake itakuwa ni nini?”

13 Malaika waBwanaakamjibu, “Mke wako hana budi kufanya yale yote niliyomwambia.

14 Kamwe asile kitu cho chote kitakachotoka katika mzabibu, wala asinywe mvinyo wa aina yo yote wala kileo cho chote wala asile kitu cho chote kilicho najisi. Hana budi kufanya kila kitu nilichomwagiza.”

15 Manoa akamjibu yule malaika waBwana, “Twakuomba usubiri kwanza ili tuweze kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako.”

16 Malaika waBwanaakamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula cho chote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtoleeBwanahiyo sadaka.” (Kwa kuwa Manoa hakujua kuwa alikuwa malaika waBwana.)

17 Ndipo Manoa akamwuliza yule malaika waBwana, “Jina lako ni nani, ili kwamba tuweze kukupa heshima hapo hayo uliyonena yatakapotimia?”

18 Akamjibu, “Kwa nini unauliza Jina langu? Ni Jina la ajabu.”

19 Ndipo Manoa akamchukua mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, naye akamtoleaBwanadhabihu hapo juu ya mwamba. Naye yule malaika waBwanaakafanya jambo la ajabu wakati Manoa na mkewe wakiwa wanaangalia:

20 Mwali wa moto kutoka hapo madhabahuni ulipowaka kuelekea mbinguni, malaika waBwanaakapaa ndani ya huo mwali. Manoa na mkewe, kwa kuona jambo hili, wakaanguka chini kifudifudi.

21 Malaika waBwanahakumtokea tena Manoa na mkewe. Ndipo Manoa akatambua kuwa huyo alikuwa malaika waBwana.

22 Manoa akamwambia mkewe, “Hakika tutakufa, kwa kuwa tumemwona Mungu.”

23 Lakini mkewe akamwambia, “IkiwaBwanaalikuwa amekusudia kutuua, asingelipokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya unga kutoka mikononi mwetu, wala asingelituonyesha mambo haya yote wala kututangazia mambo kama haya wakati huu.”

24 Yule mwanamke akazaa mtoto wa kiume akamwita jina lake Samsoni. Kijana akakua, nayeBwanaakambariki.

25 Roho waBwanaakaanza kumsukuma wakati alipokuwa huko Mahane-Dani, kati ya Sora na Eshtaoli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JDG/13-e557ecacc6155f6b16ba1881e68206c8.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 4 =