Yona 2

Maombi ya Yona Katika Tumbo la Nyangumi

1 Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwombaBwanaMungu wake.

2 Akasema:

“Katika shida yangu nalimwitaBwana,

naye akanijibu.

# Kutoka kina cha kaburiniliomba msaada,

nawe ukasikiliza kilio changu.

3 Ulinitupa kwenye kilindi,

ndani kabisa ya moyo wa bahari,

mikondo ya maji ilinizunguka,

mawimbi yako yote na viwimbi

vilipita juu yangu.

4 Nikasema, ‘Nimefukuziwa

mbali na uso wako,

hata hivyo nitatazama tena

kuelekea Hekalu lako takatifu.’

5 Maji yaliyonimeza yalinitisha,

kilindi kilinizunguka;

# mwaniulijisokota kichwani pangu.

6 Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,

makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.

Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,

EeBwanaMungu wangu.

7 “Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,

nilikukumbuka wewe,Bwana,

nayo maombi yangu yalikufikia wewe,

katika Hekalu lako takatifu.

8 “Wale watu wanaong’ang’ana na sanamu zisizofaa

hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.

9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

nitakutolea dhabihu.

Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

Wokovu watoka kwaBwana.”

10 BasiBwanaakamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JON/2-1ef80839c1ff5f108dbc49b6c823801f.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 5 =