Zaburi 9

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Muth-Labeni

#

. Zaburi Ya Daudi)

1 EeBwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,

nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

2 Nitafurahi na kushangilia katika wewe,

nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.

3 Adui zangu wamerudi nyuma,

wamejikwaa na kuangamia mbele zako.

4 Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu;

umeketi kwenye kiti chako cha enzi,

ukihukumu kwa haki.

5 Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu;

umeyafuta majina yao milele na milele.

6 Uharibifu usiokoma umempata adui,

umeing’oa miji yao,

hata kumbukumbu lao limetoweka.

7 Bwanaanatawala milele,

ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.

8 Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki,

atatawala mataifa kwa haki.

9 Bwanani kimbilio la watu wanaoonewa,

ni ngome imara wakati wa shida.

10 Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,

kwa maana weweBwana,

hujawaacha kamwe wakutafutao.

11 MwimbieniBwanasifa, amefanywa mtawala Sayuni,

tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.

12 Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka,

hapuuzi kilio cha wanaoonewa.

13 EeBwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!

Unihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

14 ili niweze kutangaza sifa zako

katika malango ya Binti Sayuni

na huko niushangilie wokovu wako.

15 Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba,

miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.

16 Bwanaanajulikana kwa haki yake,

waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

17 Waovu wataishia kuzimu,

naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

18 Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote,

wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.

19 EeBwana, inuka, usimwache binadamu ashinde,

mataifa na yahukumiwe mbele zako.

20 EeBwana, wapige kwa hofu,

mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/9-0f5efef9c3685c2abd60fe6eb0bef333.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 5 =