Zekaria 13

Kutakaswa Dhambi

1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.

2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.

3 Ikiwa yupo ye yote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina laBwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.

4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu.

5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’

6 Ikiwa mtu atamwuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’

Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika

7 “Amka, Ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu,

dhidi ya mtu aliye karibu nami!”

asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Mpige mchungaji,

nao kondoo watatawanyika,

nami nitageuza mkono wangu

dhidi ya walio wadogo,

8 katika nchi yote,” asemaBwana,

“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;

hata hivyo theluthi moja watabakia ndani yake.

9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto;

nitawasafisha kama fedha isafishwavyo

na kuwajaribu kama dhahabu.

Wataliitia Jina langu

nami nitawajibu;

nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’

nao watasema, ‘Bwanani Mungu wetu.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/13-e23899078fb1e45117b740bf03ba066c.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − 1 =