Zekaria 6

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba!

2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi,

3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu.

4 Nikamwuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”

5 Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake.

6 Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”

7 Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

8 Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.”

Taji Kwa Ajili Ya Yoshua

9 Neno laBwanalikanijia kusema:

10 “Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania.

11 Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa Kuhani Mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki.

12 Umwambie, hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu laBwana.

13 Ni yeye atakayejenga Hekalu laBwana, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’

14 Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu laBwana.

15 Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu laBwana, nanyi mtajua ya kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtiiBwanaMungu wenu kwa bidii.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/6-37bf2cdc07051c6c342943793dc898da.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

6 + seven =