1 Samweli 21

Daudi Huko Nobu 1 Daudi akaenda Nobu, kwa Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akatetemeka alipokutana naye, akamwuliza, “Kwa nini uko peke yako? Kwa nini hukufuatana na mtu ye yote?” 2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, “Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu ye yote asijue cho chote kuhusu kazi yake wala maagizo yako!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia […]

1 Samweli 22

Daudi Akiwa Adulamu Na Mispa 1 Daudi akaondoka Gathi na kukimbilia kwenye pango la Adulamu. Ndugu zake na watu wa nyumba ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 2 Wale wote waliokuwa katika dhiki au waliokuwa na madeni au wale ambao hawakuridhika wakamkusanyikia Daudi, naye akawa kiongozi wao. Watu wapatao 400 walikuwa pamoja naye. […]

1 Samweli 23

Daudi Aokoa Keila 1 Daudi alipoambiwa kuwa, “Tazama, Wafilisti wanapigana dhidi ya Keila nao wanapokonya nafaka katika sakafu za kupuria,” 2 akauliza kwaBwana, akisema, “Je, niende na kuwashambulia hawa Wafilisti?” Bwanaakamjibu, “Nenda, washambulie Wafilisti na uiokoe Keila.” 3 Lakini watu wa Daudi wakamwambia, “Hapa Yuda kwenyewe tunaogopa. Si zaidi sana, kama tukienda Keila dhidi ya […]

1 Samweli 24

Daudi Amwacha Sauli Hai 1 Baada ya Sauli kurudi kuwafuatia Wafilisti, akaambiwa kwamba, “Daudi yuko katika Jangwa la En-Gedi.” 2 Basi Sauli akachukua watu hodari 3,000 kutoka Israeli yote kwenda kumsaka Daudi na watu wake karibu na Majabali ya Mbuzi Mwitu. 3 Akaja mpaka kwenye mazizi ya kondoo kando ya njia, hapo palikuwa na pango, […]

1 Samweli 25

Daudi, Nabali Na Abigaili 1 Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akatelemka kwenye Jangwa la Maoni. 2 Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na mali huko Karmeli, yeye alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli. 3 […]

1 Samweli 26

Daudi Amwacha Sauli Hai Tena 1 Hao Wazifu wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kinachotazamana na Yeshimoni?” 2 Hivyo Sauli akashuka kwenda katika Jangwa la Zifu, akiwa na watu wake 3,000 wa Israeli waliochaguliwa, kumsaka Daudi huko. 3 Sauli akapiga kambi yake kando ya barabara juu ya kilima […]

1 Samweli 27

Daudi Miongoni Mwa Wafilisti 1 Daudi akasema moyoni mwake, “Katika mojawapo ya siku hizi nitaangamizwa kwa mkono wa Sauli. Jambo lililo bora ni kutorokea kwenye nchi ya Wafilisti. Hivyo Sauli atakata tamaa ya kunisaka po pote katika Israeli, nami nitakuwa nimeponyoka mkononi mwake.” 2 Hivyo Daudi akaondoka na hao watu mia sita waliokuwa pamoja naye […]

1 Samweli 28

Sauli Na Mchawi Wa Endori 1 Siku zile Wafilisti wakakusanya majeshi yao ili kupigana vita dhidi ya Israeli. Akishi akamwambia Daudi, “Lazima ujue kuwa wewe pamoja na watu wako mtafuatana nami kwenda vitani.” 2 Daudi akasema, “Ndipo wewe mwenyewe utakapojionea jambo ambalo mtumishi wako anaweza kufanya.” Akishi akamjibu Daudi, “Vyema sana, mimi nitakufanya uwe mlinzi […]

1 Samweli 29

Akishi Amrudisha Daudi Huko Siklagi 1 Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki, nao Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli. 2 Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi. 3 Majemadari wa Wafilisti wakauliza, “Vipi kuhusu […]

1 Samweli 30

Daudi Aangamiza Waamaleki 1 Daudi na watu wake wakafika Siklagi siku ya tatu. Basi Waamaleki walikuwa wamevamia Negebu na Siklagi. Wakawa wameshambulia mji wa Siklagi na kuuteketeza kwa moto, 2 nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua ye yote, bali waliwachukua wakaenda zao. 3 Daudi na watu wake […]