1 Samweli 31

Sauli Ajiua 1 Basi Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, na wengi wakauawa kwenye Mlima wa Gilboa. 2 Wafilisti wakawasonga Sauli na wanawe kwa nguvu, na kuwaua wanawe Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. 3 Mapigano yakawa makali sana kumzunguka Sauli, nao wapiga upinde wakampata na kumjeruhi vibaya. 4 Sauli akamwambia mchukua silaha […]