Mwanzo 41

Ndoto Za Farao 1 Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Nile, 2 wakati ng’ombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye manyasi. 3 Baada yao ng’ombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Nile wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. 4 Wale ng’ombe […]

Mwanzo 42

Ndugu Za Yosefu Waenda Misri 1 Wakati Yakobo alipofahamu kuwa kuna nafaka huko Misri, akawaambia wanawe, “Mbona mnakaa tu hapa mnatazamana?” 2 Akaendelea kuwaambia, “Nimesikia kuwa huko Misri kuna nafaka. Telemkeni huko mkanunue chakula kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi wala tusife.” 3 Ndipo wale ndugu kumi wa Yosefu, wakatelemka huko Misri kununua nafaka. 4 […]

Mwanzo 43

Safari Ya Pili Ya Kwenda Misri 1 Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi. 2 Hivyo wakati walipokuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.” 3 Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu […]

Mwanzo 44

Kikombe Cha Fedha Ndani Ya Gunia 1 Kisha Yosefu akampa yule msimamizi wa nyumbani mwake maagizo haya: “Jaza magunia ya watu hawa kiasi cha chakula ambacho wanaweza kuchukua, na uweke fedha ya kila mtu kwenye mdomo wa gunia lake. 2 Kisha weka kikombe changu kile cha fedha kwenye mdomo wa gunia la yule mdogo wa […]

Mwanzo 45

Yosefu Anajitambulisha 1 Hapo Yosefu hakuweza kujizuia zaidi mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye, akapaza sauti, akasema, “Mwondoeni kila mtu mbele yangu!” Kwa hiyo hapakuwepo mtu ye yote pamoja na Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari. […]

Mwanzo 46

Yakobo Aenda Misri 1 Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake. 2 Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!” Akajibu, “Mimi hapa.” 3 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. […]

Mwanzo 47

Yakobo Ambariki Farao 1 Yosefu akaenda na kumwambia Farao, “Baba yangu na ndugu zangu wamekuja kutoka nchi ya Kanaani wakiwa na makundi yao ya kondoo, mbuzi na ng’ombe, pamoja na kila kitu walichonacho, nao sasa wapo huko Gosheni.” 2 Akachagua ndugu zake watano na kuwaonyesha kwa Farao. 3 Farao akawauliza hao ndugu zake, “Kazi yenu […]

Mwanzo 48

Manase Na Efraimu 1 Baada ya muda Yosefu akaambiwa kwamba, “Baba yako ni mgonjwa.” Kwa hiyo akawachukua wanawe wawili Manase na Efraimu, pamoja naye. 2 Yakobo alipoambiwa, “Mwanao Yosefu amekujia kukuona,” Israeli akakusanya nguvu zake, akaketi kitandani. 3 Yakobo akamwambia Yosefu, “Mungu Mwenyezialinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani, huko akanibariki, 4 naye akaniambia, ‘Nitakufanya […]

Mwanzo 49

Yakobo Abariki Wanawe 1 Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo. 2 “Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo, msikilizeni baba yenu Israeli. 3 “Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. 4 Usiyezuiwa […]

Mwanzo 50

1 Basi Yosefu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu. 2 Ndipo Yosefu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa ili asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze, 3 wakatumia siku arobaini, kwa maana ndio muda uliotakiwa wa kutia dawa ili asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini. 4 Siku za kumwombolezea […]