Mwanzo 21

Kuzaliwa Kwa Isaki 1 Wakati huuBwanaakamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, nayeBwanaakamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 3 Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 4 Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 5 Abrahamu alikuwa […]

Mwanzo 22

Kujua Uthabiti Wa Abrahamu 1 Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.” 2 Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” 3 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua […]

Mwanzo 23

Kifo Cha Sara 1 Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba. 2 Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, Abrahamu akamwombolezea na kumlilia Sara. 3 Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema, 4 “Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. […]

Mwanzo 24

Isaki Na Rebeka 1 Wakati huu Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, nayeBwanaalikuwa amembariki katika kila njia. 2 Akamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu, 3 Ninataka uape kwaBwana, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba […]

Mwanzo 25

Kifo Cha Abrahamu 1 Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura. 2 Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. 3 Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi. 4 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa […]

Mwanzo 26

Isaki Na Abimeleki 1 Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Abrahamu. Isaki akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. 2 Bwanaakamtokea Isaki, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. 3 Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa […]

Mwanzo 27

Yakobo Anaipata Baraka Ya Isaki 1 Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” Akajibu, “Mimi hapa.” 2 Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu. 3 Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upindi, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa […]

Mwanzo 28

1 Basi Isaki akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke wa Kikanaani. 2 Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako. 3 Mungu Mwenyezina akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya […]

Mwanzo 29

Yakobo Awasili Padan-Aramu 1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika kwenye nchi za mataifa ya mashariki. 2 Huko akaona kisima katika shamba, pamoja na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu na kisima hicho kwa sababu walikuwa wanakunywa maji kutoka kwenye kisimani hicho. Jiwe lililokuwa mdomoni mwa kisima lilikuwa kubwa. 3 Wakati kondoo wanapokuwa […]

Mwanzo 30

1 Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea ndugu yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!” 2 Yakobo akamkasirikia, akamwambia, “Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia usizae watoto?” 3 Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi […]