Waamuzi 21

Wabenyamini Watafutiwa Wake 1 Wana wa Israeli walikuwa wameapa kwa kiapo kule Mispa: “Hapana mtu awaye yote atakayemwoza binti yake kwa Wabenyamini.” 2 Watu wakaenda Betheli, wakaketi mbele za Mungu mpaka jioni, wakapaza sauti zao, wakalia sana. 3 Wakasema, “EeBwana, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limewapata Waisraeli? Kwa nini kabila moja la Israeli […]