Waamuzi 11

1 Basi Yefta Mgileadi alikuwa mtu shujaa. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba. 2 Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamaa yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” 3 Basi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika […]

Waamuzi 12

Yefta Na Efraimu 1 Watu wa Efraimu wakaita majeshi yao, wakavuka kwenda Zafoni, wakamwambia Yefta, “Kwa nini mmekwenda kupigana na Waamoni bila kutuita ili tuende pamoja nawe? Basi tutaichoma moto nyumba yako, pamoja nawe ukiwa ndani yake.” 2 Yefta akajibu, “Mimi na watu wangu tulikuwa na ugomvi mkubwa na Waamoni, hata ingawa niliwaita hamkuniokoa katika […]

Waamuzi 13

Kuzaliwa Kwa Samsoni 1 Waisraeli wakafanya maovu tena mbele zaBwana. HivyoBwanaakawatia mikononi mwa Wafilisti kwa muda wa miaka arobaini. 2 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Sora, aliyeitwa Manoa, wa kabila la Wadani, naye alikuwa na mke ambaye alikuwa tasa na hakuwa na mtoto. 3 Malaika waBwanaakamtokea huyo mwanamke na kumwambia, “Wewe ni tasa na […]

Waamuzi 14

Ndoa Ya Samsoni 1 Samsoni akatelemkia Timna, akamwona mwanamke wa Kifilisti. 2 Alipopanda kutoka huko, akawaambia baba yake na mama yake, “Nimemwona mwanamke wa Kifilisti huko Timna; basi mnipatie ili awe mke wangu.” 3 Baba yake na mama yake wakamjibu, “Je, hakuna mwanamke miongoni mwa jamaa yako au miongoni mwa ndugu zako, hata ulazimike kwenda […]

Waamuzi 15

Kisasi Cha Samsoni Kwa Wafilisti 1 Baada ya kitambo kidogo, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mwana-mbuzi, kwenda kumzuru mkewe. Akasema, “Nataka kuingia chumbani kwa mke wangu.” Lakini baba yake huyo mwanamke hakumruhusu kuingia. 2 Huyo baba mkwe wake akamwambia, “Nilikuwa na hakika kwamba ulimkataa, hivyo mimi nikampa rafiki yako. Je, mdogo wake wa […]

Waamuzi 16

Samsoni Na Delila 1 Siku moja Samsoni akaenda Gaza, akamwona huko mwanamke kahaba, naye akaingia kwake. 2 Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja huku!” Hivyo wakapazingira pale mahali nao wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji. Wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, “Tumvizie hadi mapambazuko, ndipo tutamwua.” 3 Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati […]

Waamuzi 17

Sanamu Za Mika 1 Palikuwa na mtu aliyeitwa Mika ambaye aliishi katika vilima vya Efraimu. 2 Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.” Ndipo mama yake akamwambia, “Bwanana akubariki, mwanangu.” 3 Alipozirudisha zile shekeli 1,100 za fedha kwa mama […]

Waamuzi 18

Wadani Wahamia Laishi 1 Katika siku hizo Israeli walikuwa hawana mfalme. Katika siku hizo kabila la Wadani walikuwa wanatafuta mahali pao wenyewe pa kuishi, kwa sababu walikuwa hawajafika kwenye urithi wao miongoni mwa makabila ya Israeli. 2 Hivyo Wadani wakatuma mashujaa watano kutoka Sora na Eshtaoli ili kupeleleza nchi na kuichunguza. Hawa watu waliwakilisha koo […]

Waamuzi 19

Mlawi Na Suria Wake 1 Katika siku hizo Israeli hawakuwa na mfalme. Basi Mlawi mmoja aliyeishi sehemu za mbali katika nchi ya vilima ya Efraimu, akamchukua suria mmoja kutoka Bethlehemu ya Yuda. 2 Lakini suria wake akafanya ukahaba dhidi yake, naye akamwacha akarudi nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu ya Yuda. Baada ya kukaa huko […]

Waamuzi 20

Waisraeli Wapigana Na Wabenyamini 1 Ndipo Waisraeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na wa kutoka nchi ya Gileadi wakatoka kama mtu mmoja wakakusanyika mbele zaBwanahuko Mizpa. 2 Viongozi wote wa kabila za Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, askari 400,000 waendao kwa miguu wenye panga. 3 (Wabenyamini wakasikia kuwa Waisraeli […]