Yeremia 31

Kurudi Kwa Watu Wa Uhamishoni Kwa Shangwe 1 “Wakati huo, nitakuwa Mungu wa koo zote za Israeli nao watakuwa watu wangu,” asemaBwana. 2 Hili ndilo asemaloBwana: “Watu watakaopona upanga watapata upendeleo jangwani, nitakuja niwape Israeli pumziko.” 3 Bwanaalitutokea wakati uliopita akisema: “Nimekupenda kwa upendo wa milele, nimekuvuta kwa wema. 4 Nitakujenga tena nawe utajengeka upya, […]

Yeremia 32

Yeremia Anunua Shamba 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwaBwanakatika mwaka wa kumi wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Mfalme Nebukadneza. 2 Wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka mji wa Yerusalemu, naye nabii Yeremia alikuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi […]

Yeremia 33

Ahadi Ya Kurudishwa 1 Wakati Yeremia alipokuwa angali amefungwa kwenye ua wa walinzi, neno laBwanalilimjia mara ya pili kusema: 2 “Hili ndiloBwanaasemalo, yeye aliyeumba dunia,Bwanaaliyeifanya na kuithibitisha,Bwanandilo jina lake: 3 ‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika usiyoyajua.’ 4 Kwa maana hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba katika mji huu na […]

Yeremia 34

Onyo Kwa Sedekia 1 Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walipokuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote inayoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwaBwana: 2 “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli, kusema: Nenda kwa Sedekia, mfalme wa Yuda na umwambie, ‘Hili […]

Yeremia 35

Warekabi Wasifiwa 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwaBwanawakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: 2 “Nenda kwa jamaa ya Warekabi na uwaalike waje kwenye moja ya vyumba vya pembeni vya nyumba yaBwanana uwape divai wanywe.” 3 Basi nikaenda kumwita Yaazania mwana wa Yeremia, mwana wa Habazinia, ndugu zake na […]

Yeremia 36

Yehoyakimu Achoma Kitabu Cha Yeremia 1 Katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia nabii Yeremia kutoka kwaBwanakusema: 2 “Chukua kitabu na uandike ndani yake maneno yote niliyonena nawe kuhusu Israeli, Yuda na mataifa mengine yote tangu nilipoanza kunena nawe wakati wa utawala wa Yosia hadi sasa. 3 […]

Yeremia 37

Yeremia Gerezani 1 Sedekia mwana wa Yosia akafanywa kuwa mfalme wa Yuda na Nebukadneza mfalme wa Babeli, akatawala mahali pa Yehoyakinimwana wa Yehoyakimu. 2 Lakini si Sedekia wala watumishi wake wala watu wa nchi waliosikiliza maneno yaBwanaaliyonena kupitia kwa nabii Yeremia. 3 Hata hivyo, Mfalme Sedekia, akamtuma Yehukali mwana wa Shelemia pamoja na kuhani Sefania […]

Yeremia 38

Yeremia Atupwa Kwenye Kisima 1 Shefatia mwana wa Matani, Gedalia mwana wa Pashuri, Yehukali mwana wa Shelemia na Pashuri mwana wa Malkiya wakasikia kile Yeremia alichokuwa akiwaambia watu wote wakati aliposema, 2 “Hili ndilo asemaloBwana: ‘Ye yote akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni, lakini ye yote atakayejisalimisha kwa Wakaldayo ataishi. […]

Yeremia 39

Anguko La Yerusalemu 1 Hivi ndivyo Yerusalemu ilivyotwaliwa: Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Mfalme Sedekia wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alilipeleka jeshi lake lote dhidi ya Yerusalemu na akauzunguka. 2 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia […]

Yeremia 40

Yeremia Aachiwa Huru 1 Neno likamjia Yeremia kutoka kwaBwanabaada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa kifalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli. 2 Kiongozi wa walinzi alipomwona Yeremia, akamwambia, “BwanaMungu wako aliamuru maafa haya kwa ajili ya mahali hapa. […]