Yeremia 11

Agano Limevunjwa 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwaBwana: 2 “Sikia maneno ya Agano hili, nawe uwaambie watu wa Yuda na wale waishio katika Yerusalemu. 3 Waambie kwamba hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: ‘Amelaaniwa mtu yule ambaye hatayatii maneno ya Agano hili, 4 yaani maneno niliyowaamuru baba zenu nilipowatoa katika nchi ya Misri, […]

Yeremia 12

Lalamiko La Yeremia 1 Wewe daima u mwenye haki, EeBwana, niletapo daawa mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasiowaaminifu wote wanaishi kwa raha? 2 Umewapanda nao wameota, wanakua na kuzaa matunda. Daima u midomoni mwao lakini mbali na mioyo yao. 3 Hata hivyo unanijua […]

Yeremia 13

Mkanda Wa Kitani 1 Hili ndiloBwanaaliloniambia: “Nenda ukanunue mkanda wa kitani ujivike kiunoni mwako, lakini usiuache uguse maji.” 2 Kwa hiyo nikanunua mkanda, kamaBwanaalivyoniagiza, nikajivika kiunoni. 3 Ndipo neno laBwanalikanijia kwa mara ya pili: 4 “Chukua mkanda ulionunua ambao umeuvaa kiunoni mwako, uende sasa Eufrati na ukaufiche ndani ya ufa mdogo kwenye mwamba.” 5 Ndipo […]

Yeremia 14

Ukame, Njaa Na Upanga 1 Hili ndilo neno laBwanakwa Yeremia kuhusu ukame: 2 “Yuda anaomboleza, miji yake inayodhoofika; wanaomboleza kwa ajili ya nchi, nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu. 3 Wakuu wanawatuma watumishi wao maji; wanakwenda visimani lakini humo hakuna maji. Wanarudi na vyombo bila maji; wakiwa na hofu na kukata tamaa, wanafunika vichwa vyao. 4 […]

Yeremia 15

Adhabu Isiyoepukika 1 KishaBwanaakaniambia: “Hata kama Mose na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende! 2 Nao kama wakikuuliza, ‘Tuende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndiloBwanaasemalo: “ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe; waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga; waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa: […]

Yeremia 16

Siku Ya Maafa 1 Kisha neno laBwanalikanijia: 2 “Kamwe usioe na kuwa na wana wala binti mahali hapa.” 3 Kwa maana hilo ndilo asemaloBwanakuhusu wana na binti wazaliwao katika nchi hii na kuhusu wale wanawake ambao ni mama zao na wale wanaume ambao ni baba zao: 4 “Watakufa kwa magonjwa ya kufisha. Hawataombolezewa wala kuzikwa […]

Yeremia 17

Dhambi Ya Yuda Na Adhabu yake 1 “Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma, imeandikwa kwa ncha ya almasi, kwenye vibao vya mioyo yao na kwenye pembe za madhabahu zao. 2 Hata watoto wao wanakumbuka madhabahu zao # na nguzo za Ashera kandokando ya miti iliyotanda na juu ya vilima virefu. 3 Mlima wangu […]

Yeremia 18

Katika Nyumba Ya Mfinyanzi 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwaBwana: 2 “Shuka uende mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nami huko nitakupa ujumbe wangu.” 3 Kwa hiyo nikashuka mpaka kwenye nyumba ya mfinyanzi, nikamkuta akifinyanga kwa gurudumu lake. 4 Lakini chombo alichokuwa akikifinyanga kutokana na udongo kilivunjika mikononi mwake, hivyo mfinyanzi akakifanya kuwa chombo […]

Yeremia 19

Gudulia La Udongo Lililovunjika 1 Hili ndilo asemaloBwana: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kutoka kwa mfinyanzi. Wachukue baadhi ya wazee wa watu na wa makuhani 2 na mtoke mwende mpaka kwenye Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia, 3 nawe useme, ‘Sikieni neno laBwana, enyi wafalme wa Yuda […]

Yeremia 20

Yeremia Ateswa Na Pashuri 1 Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu laBwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya, 2 akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa katika mkatale katika Lango la Juu la Benyamini katika Hekalu laBwana. 3 Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwanahakukuita […]