1 Mambo ya Nyakati 22

1 Ndipo Daudi akasema, “Nyumba yaBwanaMungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”

Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu

2 Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu.

3 Akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika.

4 Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi, idadi kubwa ya mierezi.

5 Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili yaBwanainatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.

6 Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili yaBwana, Mungu wa Israeli.

7 Daudi akamwambia Solomoni, “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina laBwanaMungu wangu.

8 Lakini neno hili laBwanalikanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu.

9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake.

10 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’

11 “Sasa, mwanangu,Bwanaawe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba yaBwanaMungu wako, kama alivyosema utafanya.

12 Bwanana akupe hekima na ufahamu wakati atakapokuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria yaBwanaMungu wako.

13 Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheriaBwanaalizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.

14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu laBwanatalanta 100,000za dhahabu, talanta 1,000,000za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.

15 Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi

16 wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, nayeBwanaawe pamoja nawe.”

17 Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe.

18 Akawaambia, “Je,BwanaMungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini yaBwanana watu wake.

19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafutaBwanaMungu wenu. Anzeni kujenga Maskani yaBwanaMungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano laBwanana vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina laBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/22-14fdb82cc0317ac3f353dcf4b04e6161.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one + 15 =