1 Mambo ya Nyakati 21

Daudi Ahesabu Wapiganaji

1 Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli.

2 Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.”

3 Yoabu akajibu, “Bwanana aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raia wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?”

4 Hata hivyo, neno la mfalme, likawa na nguvu juu ya Yoabu; kwa hiyo Yoabu akaondoka na kuzunguka Israeli yote kisha akarudi Yerusalemu.

5 Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000.

6 Lakini Yoabu hakuwahesabu Walawi na Wabenyamini, kwa sababu alichukizwa sana na amri ya mfalme.

7 Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia, hivyo akaiadhibu Israeli.

8 Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya hivi. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

9 Bwanaakamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi,

10 “Nenda ukamwambie Daudi, hili ndilo asemaloBwana, ‘ninakupa kuchagua miongoni mwa mambo matatu. Chagua mojawapo ili nipate kulitenda dhidi yako.’ ”

11 Kwa hiyo Gadi akamwendea Daudi akamwambia, “Hili ndiloBwanaasemalo: ‘Chagua:

12 miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga waBwana, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika waBwanaakiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”

13 Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwaBwanakwa sababu rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”

14 BasiBwanaakapeleka tauni juu ya Israeli, watu 70,000 wa Israeli wakafa.

15 Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo,Bwanaakaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Sasa rudisha mkono wako.” Wakati huu huyu malaika waBwanaalikuwa amesimama katika uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.

16 Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika waBwanaakiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.

17 Daudi akamwambia Mungu, “Je, si mimi ndiye niliyeamuru watu wahesabiwe? Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Kwani wao wamekosa nini? EeBwana, Mungu wangu, mkono wako na uwe juu yangu mimi na jamaa yangu, lakini usiache tauni hii iendelee juu ya watu wako.”

18 Kisha malaika waBwanaakamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengeaBwanamadhabahu katika uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.

19 Kwa hiyo Daudi akakwea akalitii lile neno ambalo Gadi alikuwa amelisema katika jina laBwana.

20 Wakati Arauna alipokuwa anapura ngano, akageuka akamwona yule malaika. Wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha, yeye akaendelea kupura ngano

21 Kisha Daudi akakaribia, Arauna alipotazama na kumwona, akaondoka kwenye uwanja wa kupuria nafaka akamsujudia Daudi akainamisha uso wake mpaka chini.

22 Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu yaBwanatauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”

23 Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lo lote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”

24 Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili yaBwanaau kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu cho chote.”

25 Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600kwa ajili ya ule uwanja.

26 Kisha Daudi akamjengeaBwanamadhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kutekezwa na sadaka za amani. AkamwitaBwananayeBwanaakajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.

27 KishaBwanaakanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake.

28 Wakati huo, Daudi alipoona kwambaBwanaamemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi, akatoa dhabihu huko.

29 Maskani yaBwanaambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni.

30 Lakini Daudi hakuthubutu kuisogelea ili kumwuliza Mungu, kwa sababu aliuogopa upanga wa yule malaika waBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/21-e96ee7b0f42df3da8e18f62f51d356e8.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five − three =