1 Samweli 14

1 Siku moja Yonathani mwana wa Sauli akamwambia kijana mbeba silaha wake, akasema, “Njoo, tuwavukie Wafilisti kwenye doria upande ule mwingine.” Lakini hakumwambia baba yake.

2 Sauli alikuwa akikaa kwenye viunga vya Gibea chini ya mkomamanga huko Migroni. Alikuwa pamoja na watu kama 600,

3 miongoni mwao alikuwepo Ahiya, ambaye alikuwa amevaa kisibau. Alikuwa mwana wa Ikabodi, nduguye Ahitubu mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani waBwanahuko Shilo. Hakuna ye yote aliyekuwa na habari kwamba Yonathani alikuwa ameondoka.

4 Kila upande wa njia ambayo Yonathani alikusudia kupita ili kuvuka kufikia doria ya Wafilisti kulikuwepo na jabali, jabali moja lilikuwa linaitwa Bosesi na jingine Sene.

5 Jabali moja lilisimama kaskazini kuelekea Mikmashi na jingine upande wa kusini kuelekea Geba.

6 Yonathani akamwambia kijana wake mbeba silaha, “Njoo, tuvukie doria ya wale jamaa wasiotahiriwa. HuendaBwanaatatenda kwa ajili yetu. Hakuna cho chote kitakachoweza kumzuiaBwanakuokoa, kwamba ni kwa wingi au kwa uchache.”

7 Mbeba silaha wake akamwambia, “Fanya yale yote uliyonayo katika moyo wako. Songa mbele; moyo wangu na roho yangu viko pamoja nawe.”

8 Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone.

9 Kama wakituambia, ‘Subirini hapo mpaka tuje kwenu,’ tutakaa pale tulipo na hatutakwea kwao.

10 Lakini kama watasema, ‘Pandeni mje kwetu,’ tutakwea, kwa sababu hiyo itakuwa ishara yetu kwambaBwanaamewatia mikononi mwetu.”

11 Basi wote wawili wakajionyesha kwa doria ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, “Tazama! Waebrania wanatambaa toka mashimoni walimokuwa wamejificha.”

12 Watu wa kwenye doria wakawapigia kelele Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njoni pandeni kwetu nasi tutawakomesha.”

Basi Yonathani akamwambia mbeba silaha wake, “Panda nyuma yangu,Bwanaamewatia mikononi mwa Israeli.”

13 Yonathani akapanda juu, akitumia mikono yake na miguu, pamoja na mbeba silaha wake papo hapo nyuma yake. Wafilisti wakaanguka mbele ya Yonathani, naye mbeba silaha wake akamfuata akiwaua nyuma yake.

14 Katika hilo shambulio la kwanza, Yonathani na mbeba silaha wake waliua kama watu ishirini kwenye eneo kama la nusu eka.

Israeli Wawafukuza Wafilisti

15 Kisha fadhaa ikawapata jeshi lote, wale waliokuwa kambini na shambani, wale waliokuwa katika doria na makundi ya washambuliaji, nayo nchi ilitetemeka. Ilikuwa ni hofu ya ghafula iliyotumwa na Mungu.

16 Wapelelezi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona jeshi likitokomea pande zote.

17 Ndipo Sauli akawaambia watu wale waliokuwa pamoja naye, “Kagueni jeshi mkaone ni nani ameondoka katikati yetu.” Walipokagua, akawa ni Yonathani na mbeba silaha wake ambao hawakuwepo.

18 Sauli akamwambia Ahiya, “Leta Sanduku la Mungu.” (Wakati huo lilikuwa kwa Waisraeli.)

19 Wakati Sauli alipokuwa akisema na kuhani, makelele katika kambi ya Wafilisti yakaongezeka zaidi na zaidi. Hivyo Sauli akamwambia kuhani, “Rudisha mkono wako.”

20 Kisha Sauli na watu wake wote wakakusanyika na kwenda vitani. Wakawakuta Wafilisti wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, wakitiana panga kila mmoja na wenzake.

21 Wale Waebrania ambao walishakuwa pamoja na Wafilisti, na ambao walikuwa wamepanda pamoja nao katika kambi zao, wakaenda upande wa Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani.

22 Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika nchi ya milima ya Efraimu waliposikia kuwa Wafilisti wamekimbia, wakajiunga vitani na kuwafuata kwa bidii.

23 HivyoBwanaakawaokoa Waisraeli siku ile, navyo vita vilienea hadi kupita Beth-Aveni.

Yonathani Ala Asali

24 Basi watu wa Israeli walikuwa katika dhiki siku ile, kwa sababu Sauli alikuwa amewafunga watu kwa kiapo, akisema, “Alaaniwe mtu ye yote ambaye atakula chakula kabla ya jioni, kabla sijalipiza kisasi juu ya adui zangu!” Kwa hiyo hakuna mtu ye yote katika jeshi aliyeonja chakula.

25 Jeshi lote liliingia mwituni, na huko kulikuwepo na asali ardhini.

26 Walipoingia mwituni, wakaona asali ikitiririka, hata hivyo hakuna mtu ye yote aliyetia mkono wake kinywani, kwa sababu waliogopa kiapo.

27 Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kuwa baba yake alikuwa amewafunga watu kwa kiapo, hivyo akainyosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya katika sega la asali. Akainua mkono wake na kuutia kinywani mwake, nayo macho yake yakawa maangavu.

28 Kisha mmoja wa askari wake akamwambia, “Baba yako alilifunga jeshi kwa kiapo kikali, akisema, ‘Alaaniwe mtu ye yote alaye chakula leo!’ Ndiyo sababu watu wanalegea.”

29 Yonathani akasema, “Baba yangu ameitaabisha nchi. Ona jinsi nilivyopata nguvu mpya nilipoonja asali hii kidogo.

30 Ingekuwa bora zaidi mara ngapi kama watu wangalikula leo baadhi ya nyara walizoteka kutoka kwa adui zao. Je, mauaji ya Wafilisti yasingekuwa makubwa zaidi?”

31 Siku ile baada ya Waisraeli kuwaua Wafilisti kutoka Mikmashi mpaka Aiyaloni, walikuwa wamechoka.

32 Watu wakarukia zile nyara, wakichukua kondoo, ng’ombe na ndama, wakawachinja hapo juu ya nchi na kuwala, pamoja na damu.

33 Kisha mtu mmoja akamwambia Sauli, “Tazama, watu wanatenda dhambi dhidi yaBwanakwa kula nyama yenye damu ndani yake.”

Akasema, “Mmevunja uaminifu. Livingirisheni jiwe kubwa hapa mara moja.”

34 Kisha akasema, “Nendeni miongoni mwa watu na waambieni, ‘Kila mmoja wenu aniletee ng’ombe wake na kondoo, wachinjeni hapa na mle. Msitende dhambi dhidi yaBwana, kwa kula nyama ikiwa na damu ndani yake.’ ”

Hivyo kila mmoja akaleta ng’ombe wake jioni ile na kumchinja hapo.

35 Ndipo Sauli akamjengeaBwanamadhabahu, na ndiyo ilivyokuwa mara yake ya kwanza kujenga madhabahu.

36 Sauli akasema, “Tutelemke tufuatie Wafilisti usiku na kuwateka nyara mpaka mapambazuko, nasi tusiache hata mmoja wao hai.”

Wakajibu, “Fanya lo lote lile uonalo jema zaidi kwako.”

Lakini kuhani akasema, “Tuulize kwa Mungu mahali hapa.”

37 Basi Sauli akamwuliza Mungu, akisema, “Je, nitelemke kuwafuatia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwa Israeli?” Lakini Mungu hakumjibu siku ile.

38 Kwa hiyo Sauli akasema, “Njoni hapa, ninyi nyote ambao ni viongozi wa jeshi, na tutafute ni dhambi gani imefanywa leo.

39 Kwa hakika kamaBwanaaiokoaye Israeli aishivyo, hata kama itakuwa juu ya mwana wangu Yonathani, ni lazima afe.” Lakini hakuna mtu ye yote aliyesema neno.

40 Kisha Sauli akawaambia Waisraeli wote, “Ninyi simameni huko; mimi na mwanangu Yonathani tutasimama hapa.”

Watu wakajibu, “Fanya lile unaloona jema zaidi kwako.”

41 Kisha Sauli akamwombaBwana, Mungu wa Israeli, akisema, “Nipe jibu lililo sawa.” Yonathani na Sauli wakatolewa kwa kura, nao watu wakawa salama.

42 Sauli akasema, “Pigeni kura kati yangu na mwanangu Yonathani.” Kura ikamwangukia Yonathani.

43 Basi Sauli akamwambia Yonathani, “Niambie ni nini ulichokifanya.”

Hivyo Yonathani akamwambia, “Nilionja tu asali kidogo kwa ncha ya fimbo yangu, Je, sasa ni lazima nife?”

44 Sauli akasema, “Mungu na anishughulikie kwa ukali zaidi kama wewe Yonathani hutakufa.”

45 Lakini watu wakamwambia Sauli, “Je, Yonathani atakufa, yeye ambaye ameleta wokovu huu mkubwa Israeli? Hasha! Hakika kamaBwanaaishivyo, hakuna hata unywele wa kichwa chake utakaoanguka juu ya ardhi, kwa kuwa alifanya jambo hili leo kwa msaada wa Mungu.” Basi watu wakamwokoa Yonathani, wala hakuuawa.

46 Kisha Sauli akaacha kuwafuata Wafilisti, nao wakajiondoa na kurudi katika nchi yao.

47 Baada ya Sauli kujitwalia utawala katika Israeli, alipigana dhidi ya adui zake kila upande: Moabu, Waamoni, Edomu, wafalme wa Soba, na Wafilisti. Po pote alipogeukia, aliwashinda.

48 Akapigana kishujaa na kuwashinda Waamaleki, akiikomboa Israeli kutoka katika mikono ya wale ambao walikuwa wamewateka nyara.

Jamaa Ya Sauli

49 Wana wa Sauli walikuwa Yonathani, Ishvi na Malki-Shua. Jina la binti yake mkubwa aliitwa Merabu, na mdogo aliitwa Mikali.

50 Jina la mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu binti wa Ahimaasi. Jina la jemadari wa jeshi la Sauli aliitwa Abneri mwana wa Neri, naye Neri alikuwa babaye mdogo Sauli.

51 Babaye Sauli yaani, Kishi na Neri baba yake Abneri walikuwa wana wa Abieli.

52 Siku zote za kutawala kwa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wo wote Sauli alipomwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1SA/14-55a7bac9810ae3dd74f8b23d12b13b31.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × 1 =