1 Samweli 15

Bwana Anamkataa Sauli Asiwe Mfalme

1 Samweli akamwambia Sauli, “Mimi ndiye ambayeBwanaalinituma nikutie mafuta uwe mfalme juu ya watu wake Israeli, basi sasa sikiliza ujumbe kutoka kwaBwana.

2 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipopanda kutoka Misri.

3 Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie, waue wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”

4 Ndipo Sauli akawaita watu na kuwapanga huko Telaimu, askari wa miguu 200,000 pamoja na watu 10,000 kutoka Yuda.

5 Sauli akaenda katika mji wa Amaleki na kuwavizia bondeni.

6 Kisha akawaambia Wakeni, “Ondokeni, waacheni Waamaleki ili kwamba nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao, kwa kuwa ninyi mliwatendea mema Waisraeli wote wakati walipopanda toka Misri.” Basi Wakeni wakaondoka wakawaacha Waamaleki.

7 Ndipo Sauli akawashambulia Waamaleki toka Havila mpaka Shuri, hadi mashariki ya Misri.

8 Akamchukua Agagi, mfalme wa Waamaleki akiwa hai, nao watu wake wote akawaangamiza kabisa kwa upanga.

9 Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ng’ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

10 Kisha neno laBwanalikamjia Samweli kusema:

11 “Ninasikitika kwamba nimemfanya Sauli kuwa mfalme, kwa sababu ameacha kunifuata mimi na hakutimiza maagizo yangu.” Samweli akafadhaika, naye akamliliaBwanausiku ule wote.

12 Asubuhi na mapema Samweli akaamka kwenda kukutana na Sauli, lakini akaambiwa, “Sauli amekwenda Karmeli. Huko amesimamisha mnara kwa heshima yake mwenyewe naye ameendelea na kutelemkia Gilgali.”

13 Samweli alipomfikia, Sauli akamwambia, “Bwanaakubariki! Nimetimiza yaleBwanaaliyoniagiza.”

14 Lakini Samweli akasema, “Nini basi huu mlio wa kondoo masikioni mwangu? Huu mlio wa ng’ombe ninaousikia ni kitu gani?”

15 Sauli akajibu, “Askari wamewaleta kutoka kwa Waamaleki, waliwaacha wale kondoo na ng’ombe wazuri ili kuwatoa dhabihu kwaBwana, Mungu wako, lakini tuliwaangamiza kabisa wengine wote.”

16 Samweli akamwambia Sauli, “Ngoja! Nami nitakuambia lileBwanaaliloniambia usiku huu.”

Sauli akajibu, “Niambie.”

17 Samweli akamwambia, “Ingawa zamani ulijiona mdogo machoni pako mwenyewe, Je, hukuwa kiongozi wa kabila za Israeli?Bwanaalikutia mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli.

18 Naye akakutuma kwa kazi maalum, akisema, ‘Nenda ukaangamize kabisa wale watu waovu, wale Waamaleki, upigane nao vita mpaka utakapowaangamiza kabisa.’

19 Kwa nini hukumtiiBwana? Kwa nini ulivamia nyara na kufanya uovu machoni paBwana?”

20 Sauli akasema, “Lakini nilimtiiBwana. Nilikamilisha ile kaziBwanaaliyonituma. Niliwaangamiza Waamaleki kabisa na kumleta Agagi mfalme wao.

21 Askari walichukua kondoo na ng’ombe kutoka kwenye nyara, zile ambazo ni nzuri sana zimewekwa wakfu kwa Mungu, ili zitolewe dhabihu kwaBwanaMungu wako huko Gilgali.”

22 Lakini Samweli akajibu:

“Je,Bwanaanafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

kama vile kuitii sauti yaBwana?

Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu,

nako kusikia ni bora

kuliko mafuta ya kondoo dume.

23 Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

Kwa sababu umelikataa neno laBwana,

naye amekukataa wewe

kuendelea kuwa mfalme.”

24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri yaBwanana maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka.

25 Sasa ninakusihi, usamehe dhambi yangu nawe urudi pamoja nami, ili nipate kumwabuduBwana.”

26 Lakini Samweli akamwambia, “Sitarudi pamoja nawe. Umelikataa neno laBwana, naweBwanaamekukataa wewe usiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli!”

27 Samweli alipogeuka ili aondoke, Sauli akang’ang’ania pindo la joho lake, nalo likararuka.

28 Samweli akamwambia, “Bwanaameurarua ufalme wa Israeli kutoka kwako leo, naye ameutia kwa mmoja wa majirani zako, aliye bora kuliko wewe.

29 Yeye aliye Utukufu wa Israeli hasemi uongo wala hana kigeugeu, kwa kuwa yeye si mwanadamu, hata abadili nia yake.”

30 Sauli akajibu, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali niheshimu mbele ya wazee wa watu wangu na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, ili nipate kumwabuduBwanaMungu wako.”

31 Hivyo Samweli akarudi pamoja na Sauli, naye Sauli akamwabuduBwana.

32 Ndipo Samweli akasema, “Niletee Agagi mfalme wa Waamaleki.”

Agagi akaja kwake kwa ujasiri, akifikiri, “Hakika uchungu wa mauti umepita.”

33 Lakini Samweli akasema,

“Kama upanga wako ulivyofanya wanawake

kufiwa na watoto wao,

ndivyo mama yako atakavyokuwa

hana mtoto miongoni mwa wanawake.”

Naye Samweli akamwua Agagi mbele zaBwanahuko Gilgali.

34 Kisha Samweli akaenda Rama, lakini Sauli akapanda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli.

35 Hadi siku Samweli alipokufa hakwenda kumwona Sauli tena, ingawa Samweli alimwombolezea. NayeBwanaalihuzunika kwamba alimfanya Sauli kuwa mfalme juu ya Israeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1SA/15-d85ba7ed12adc5f74311c7e833e73f25.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × three =