1 Samweli 7

1 Kisha watu wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku laBwana. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu juu kilimani na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku laBwana.

Samweli Awatiisha Wafilisti Huko Mispa

2 Sanduku laBwanalilibakia huko Kiriath-Yearimu kwa muda mrefu, yaani jumla ya miaka ishirini, nao watu wa Israeli wakaomboleza na kumtafutaBwana.

3 Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudiaBwanakwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwaBwanana kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.”

4 Hivyo Waisraeli wakaweka mbali Mabaali yao na Maashtorethi, nao wakamtumikiaBwanapeke yake.

5 Kisha Samweli akasema, “Wakusanyeni Israeli wote huko Mispa, nami nitawaombea ninyi kwaBwana.”

6 Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele zaBwana. Siku hiyo walifunga na wakaungama, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi yaBwana.” Naye Samweli alikuwa kiongoziwa Israeli huko Mispa.

7 Wafilisti waliposikia kwamba Israeli wamekusanyika huko Mispa, watawala wa Wafilisti wakapanda ili kuwashambulia. Waisraeli waliposikia habari hiyo, waliogopa kwa sababu ya Wafilisti.

8 Wakamwambia Samweli, “Usiache kumliliaBwana, Mungu wetu kwa ajili yetu, ili kwamba apate kutuokoa na mikono ya Wafilisti.”

9 Kisha Samweli akamchukua mwana-kondoo anyonyaye na kumtoa mzima kama sadaka ya kuteketezwa kwaBwana. AkamliliaBwanakwa niaba ya Israeli, nayeBwanaakamjibu.

10 Wakati Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ileBwanaalinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli.

11 Watu wa Israeli wakatoka mbio huko Mispa na kuwafuatia Wafilisti, wakiwachinja njiani hadi mahali chini ya Beth-Kari.

12 Ndipo Samweli akachukua jiwe na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita Ebenezeri, akisema, “Hata sasaBwanaametusaidia.”

13 Basi Wafilisti wakashindwa na hawakuvamia nchi ya Israeli tena.

Katika maisha yote ya Samweli, mkono waBwanaulikuwa dhidi ya Wafilisti.

14 Miji kuanzia Ekroni hadi Gathi ile ambayo Wafilisti walikuwa wameiteka kutoka Israeli ilirudishwa kwake, nayo Israeli akazikomboa nchi za jirani kutoka mikononi mwa Wafilisti. Kukawepo amani kati ya Israeli na Waamori.

15 Samweli akaendelea kama mwamuzi juu ya Israeli siku zote za maisha yake.

16 Mwaka hadi mwaka aliendelea kuzunguka kutoka Betheli mpaka Gilgali na Mispa, akiamua Israeli katika sehemu hizo zote.

17 Lakini kila mara alirudi Rama, ambako ndiko kulikokuwa nyumbani kwake, huko pia aliwaamua Israeli. Naye huko alimjengeaBwanamadhabahu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1SA/7-8b441ad35427c44bf58cb20459f1bda5.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen + sixteen =