1 Wafalme 16

1 Ndipo neno laBwanalikamjia Yehu mwana wa Hanani dhidi ya Baasha, kusema:

2 “Nilikuinua kutoka mavumbini na kukufanya kiongozi wa watu wangu Israeli, lakini ukaenenda katika njia za Yeroboamu na kusababisha watu wangu Israeli kutenda dhambi na kunikasirisha kwa dhambi zao.

3 Basi nitamwangamiza Baasha pamoja na nyumba yake, nami nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwanawe Nebati.

4 Mbwa watawala watu wa Baasha watakaofia mjini na ndege wa angani watajilisha kwa wale watakaofia mashambani.”

5 Kwa matukio mengine ya utawala wa Baasha, aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

6 Baasha akalala na baba zake naye akazikwa huko Tirza. Naye Ela mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

7 Zaidi ya hayo, neno laBwanalikamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni paBwana, akamkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu, na pia kwa sababu aliiangamiza.

Ela Mfalme Wa Israeli

8 Katika mwaka wa ishirini na sita wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala huko Tirza kwa miaka miwili.

9 Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akafanya hila mbaya dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akilewa katika nyumba ya Arsa, mtu aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirza.

10 Zimri akaingia, akampiga na kumwua katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda. Kisha Zimri akaingia mahali pake kuwa mfalme.

11 Mara tu alipoanza kutawala na kuketi juu ya kiti cha ufalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki.

12 Hivyo Zimri akaangamiza jamaa yote ya Baasha, kulingana na neno laBwanalililonenwa dhidi ya Baasha kupitia nabii Yehu:

13 kwa sababu ya dhambi zote Baasha na mwanawe Ela walizokuwa wametenda na wakasababisha Israeli kuzitenda, basi wakamkasirishaBwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.

14 Kwa matukio mengine ya utawala wa Ela, na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

Zimri Mfalme Wa Israeli

15 Katika mwaka wa ishirini na saba wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirza siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti.

16 Wakati Waisraeli waliokuwa kambini waliposikia kuwa Zimri alikuwa amefanya hila mbaya dhidi ya mfalme na kumwua, wakamtangaza Omri, jemadari wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli siku iyo hiyo huko kambini.

17 Ndipo Omri na Waisraeli wote pamoja naye wakaondoka Gibethoni na kuizingira Tirza.

18 Wakati Zimri alipoona kuwa mji umechukuliwa, alikwenda ndani ya ngome ya jumba la kifalme na kulichoma moto jumba la kifalme na kujiteketeza ndani yake. Kwa hiyo akafa,

19 kwa sababu ya dhambi alizofanya, akitenda maovu machoni paBwanana kuenenda katika njia za Yeroboamu na katika dhambi alizofanya na kusababisha Israeli kuzifanya.

20 Kwa matukio mengine ya utawala wa Zimri, na uasi alioutenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

Omri Mfalme Wa Israeli

21 Ndipo watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamwunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme na nusu nyingine wakamwunga mkono Omri.

22 Lakini wafuasi wa Omri wakajionyesha wenye nguvu kuliko wale wa Tibni mwana wa Ginathi. Hivyo Tibni akafa na Omri akawa mfalme.

23 Katika mwaka wa thelathini na moja wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili, sita kati ya hiyo katika Tirza.

24 Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbiliza fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.

25 Lakini Omri akatenda maovu machoni paBwanana kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia.

26 Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirishaBwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.

27 Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

28 Omri akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Ahabu mwanawe akatawala mahali pake.

Ahabu Awa Mfalme Wa Israeli

29 Katika mwaka wa thelathini na nane wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na miwili.

30 Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni mwaBwanakuliko ye yote aliyewatangulia.

31 Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu.

32 Akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali lile alilolijenga huko Samaria.

33 Pia Ahabu akatengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirishaBwana, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.

34 Katika wakati wa Ahabu, Hieli, Mbetheli, akaijenga upya Yeriko. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kulingana na neno laBwanaalilosema kupitia Yoshua mwana wa Nuni.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/16-f4eadd4d8185d7ed343c7e87ef74a6e3.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two + 15 =