1 Wafalme 15

Abiya Mfalme Wa Yuda

1 Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda,

2 naye akatawala katika Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.

3 Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwaBwanaMungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.

4 Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi,BwanaMungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara.

5 Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni paBwanana hakushindwa kushika maagizo yote yaBwanasiku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.

6 Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya.

7 Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.

8 Naye Abiya akalala pamoja na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Naye Asa mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Asa Mfalme Wa Yuda

9 Katika mwaka wa ishirini wa kutawala kwake Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akawa mfalme wa Yuda,

10 naye akatawala katika Yerusalemu miaka arobaini na mmoja. Jina la bibi yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.

11 Asa akatenda yaliyo mema machoni mwaBwana, kama alivyokuwa ametenda Daudi baba yake.

12 Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka katika nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.

13 Hata akamwondoa bibi yake Maaka kwenye nafasi yake kama mama malkia, kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akakatakata hiyo nguzo na kuiteketeza kwa moto kwenye Bonde la Kidroni.

14 Japokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwaBwanakikamilifu maisha yake yote.

15 Akaleta ndani ya Hekalu laBwanafedha na dhahabu, pamoja na vitu ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

16 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zote za utawala wao.

17 Baasha mfalme wa Israeli akakwea dhidi ya Yuda na kuweka ngome Rama ili kuzuia ye yote kuingia au kutoka katika nchi ya Asa mfalme wa Yuda.

18 Kisha Asa akachukua fedha yote na dhahabu iliyokuwa imeachwa katika hazina za Hekalu laBwanana za jumba lake mwenyewe la kifalme. Akawakabidhi maafisa wake na kuwatuma kwa Ben-Hadadi mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Aramu, aliyekuwa akitawala Dameski.

19 “Akasema na pawepo mkataba kati yangu na wewe, kama ulivyokuwepo kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nakutumia zawadi ya fedha na dhahabu. Sasa vunja mkataba wako na Baasha mfalme wa Israeli ili aniache huru.”

20 Ben-Hadadi akakubaliana na Mfalme Asa na akatuma majemadari wake dhidi ya miji ya Israeli. Akaishinda miji ya Iyoni, Dani, Abel-Beth-Maaka na Kinerethi yote pamoja na Naftali.

21 Wakati Baasha aliposikia hili, akaacha kuijenga Rama na akaenda kuishi Tirza.

22 Kisha Mfalme Asa akatoa amri kwa Yuda yote, pasipo kumbagua hata mmoja, kubeba mawe na mbao kutoka Rama, ambazo Baasha alikuwa akitumia huko. Mfalme Asa akazitumia kujengea Geba iliyoko Benyamini na Mispa pia.

23 Kwa matukio yote ya utawala wa Asa, mafanikio yake yote, yote aliyofanya na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda? Katika uzee wake, hata hivyo, alipata ugonjwa wa miguu.

24 Kisha Asa akalala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoshafati mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

Nadabu Mfalme Wa Israeli

25 Nadabu mwana wa Yeroboamu akawa mfalme wa Israeli katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Asa wa Yuda, naye akatawala Israeli kwa miaka miwili.

26 Akafanya maovu machoni paBwana, akienenda katika njia za baba yake na katika dhambi yake, ambayo alisababisha Israeli kuifanya.

27 Baasha mwana wa Ahiya wa nyumba ya Isakari akafanya shauri baya dhidi yake, naye akamwua huko Gibethoni, mji wa Wafilisti, wakati Nadabu na Israeli yote walipokuwa wameuzingira.

28 Baasha akamwua Nadabu katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, naye Baasha akaingia mahali pake kuwa mfalme.

29 Mara tu alipoanza kutawala, aliua jamaa yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu ye yote aliyekuwa hai, bali aliwaangamiza wote, kulingana na neno laBwanalililotolewa kupitia kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni,

30 kwa sababu ya dhambi alizokuwa amezitenda Yeroboamu na kusababisha Israeli kuzitenda, tena kwa sababu alimkasirishaBwana, Mungu wa Israeli.

31 Kwa matukio mengine ya utawala wa Nadabu na yote aliyofanya, je hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?

32 Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli wakati wote wa utawala wao.

Baasha Mfalme Wa Israeli

33 Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya akawa mfalme wa Israeli yote huko Tirza, naye akatawala kwa miaka ishirini na minne.

34 Akatenda maovu machoni paBwana, akienenda katika njia za Yeroboamu na dhambi yake, ambayo alikuwa amesababisha Israeli kuitenda.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1KI/15-66d931e0f93b885b2650ee0b2505fed1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 + twenty =